ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 11, 2014

UN kutuma wanajeshi wa kulinda amani CAR


Kikosi cha kulinda amani cha umoja wa Afrika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepiga kura kwa kauli moja kutuma kikosi kipya cha wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati-kikosi hicho kitawajumuisha wanajeshi karibu alfu kumi na mbili.
Kwa sasa kuna wanajeshi alfu sita wa
kikosi cha umoja wa Afrika pamoja na alfu mbili kutoka Ufarnsa, lakini vikosi hivyo vimekabiliwa na wakati mgumu kurejesha utulivu.
Maelfu wamefariki duniani na takriban watu milioni moja wamelazimika kutoroka makwao kufuatia vurugu zilizodumu kipindi cha mwaka mmoja sasa.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anasema kuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na mzozo unaoibua wasiwasi-- ambapo wanamgambo wa mirengo pinzani ya kidini wanaendelea kupigana huku msimu wa mvua unaotarajiwa kuanza ukitishia zoezi la kusambaza misaada kwa waathiriwa.
Zaidi ya raia thelathini waliuwawa katika mapigano ya hivi punde katika mji wa Dekoa katikati mwa taifa hilo.
BBC

No comments: