ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 17, 2014

KINANA AWASILI WILAYA YA KALIUA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisikiliza wimbo wa mapokezi kutoka kwa wasanii wa kundi la Hiari ya Moyo mara baada ya kuwasili kwenye Jimbo la Urambo Magharibi ,wilaya ya Kaliua.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya udongo wakati wa ujunzi wa nyumba ya Daktari wa Zahanati katika kijiji cha Usindi.
 Katibu Mkuu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi  Profesa Juma Kapuya baada ya kumaliza ukaguzi wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Usindi.
 Wakina Mama wa wilaya ya Kaliua wakielekea kwenye eneo la mkutano ambapo Katibu Mkuu wa CCM  Ndugu Abdulrahman Kinana anatazamiwa kuhutubia.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mheshimiwa Samuel Sitta akisalimiana na Mbunge wa Urambo Magharibi Profesa Juma Kapuya mara baada ya kukutana wakati wa kukabidhiana ugeni unaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Uhuru .

No comments: