Wanasiasa kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini wakiwemo wabunge 17 kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ),wanatarajiwa kujiunga na chama kipya cha siasa nchini, ACT -Tanzania, kilichopata usajili wa kudumu mapema mwezi huu....
Mbali na kuwanasa wabunge hao wa CHADEMA pia kimefanikiwa kuwavuta wabunge wanne kutoka chama cha Mapinduzi ( CCM ),huku kikiwa na uhakika wa kuwachomoa wabunge watatu kutoka NNCR-Mageuzi....
Aidha ACT- Tanzania imepiga hodi ndani ya chama cha wananchi ( CUF ) ,ambapo imeshakamilisha mchakato wa kumjuimuisha kwenye safu yao ya mapambano mbunge mmoja wa viti maalumu wa chama hicho....
Taarifa za uhakika kutoka ACT- Tanzania zimeweka wazi kwamba kwenye idadi ya wabunge 17 wa CHADEMA,wabunge 6 ni wa majimbo huku wabunge 11 wakiwa ni viti maalumu.....
Kwa upande wa CCM,wabunge watatu watakaojiunga na ACT-Tanzania ni wa majimbo,huku mbunge mmoja akiwa ni wa viti maalumu.Ndani ya NNCR -Mageuzi, wabunge wote wanaotarajiwa kujiunga na chama hicho ni wa majimbo huku baadhi ya matawi ya chama hicho mkoani Kigoma nayo yakitajwa kuwa katika mchakato wa kugeuzwa kuwa ofisi za ACT-Tanzania....
Katika kuhakikisha chama hicho kinaenea katika kila kona ya nchi,tayari kimeshajiimarisha kwenye mikoa ya Kigoma,Rukwa,Katavi,Shinyanga,Lindi,Mtwara na Tabora ambapo viongozi wengi waliokuwa wakikitumia CHADEMA kuanzia ngazi za matawi hadi mikoa wameanza kufanya kazi za ACT-Tanzania....
Aidha zipo taarifa kuwa wapo baadhi ya vigogo wa CCM akiwemo waziri mkuu wa zamani wanatarajiwa kuwa wanachama wa chama hicho na kwamba bado kuna mikakati inafanyika ili kuhakikisha chama hicho kinakuwa chama chenye nguvu....
Mmoja wa viongozi wa chama cha ACT-Tanzania ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe kwa madai kuwa si msemaji wa chama hicho,alisema kwa sasa chama kimeachwa kwa vijana ili kukisambaza kwenye kila eneo na kwamba muda mwafaka ukifika kitaishangaza nchi.....
Tangu kuanzishwa kwake mapema mwaka huu,ACT- Tanzania kimeonekana kuwa chama cha upinzani cha kupambana na CHADEMA tofauti na vyama vingine ambavyo dhamira zao ni kuing'oa CCM madarakani....
Chama hicho kimekuwa kikiweka matawi yake kwenye maeneo yanayotawaliwa na CHADEMA mkoani KIGOMA na kwenye baadhi ya mikoa nchini...
Katibu wa ACT kanda ya magharibi,Wiston Moga alinukuliwa akisema kuwa lengo la chama hicho ni kuleta mabadiliko kwenye ulingo wa siasa, na wao wamedhamiria kutetea maslahi ya umma kwa lengo la kuondoa mfumo wa maslahi binafsi ambao ni chachu ya vyama vya siasa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi.....
Msemaji wa CHADEMA,Tumain Makene aliwahi kunukuliwa akisema kuwa hatua ya chama hicho kupingana na chama chao haina mantiki kwani kinaonekana kukosa mwelekeo mapema...
"Tunajua lengo lao ni lipi, wanachokifanya hakitawasaidia, ni vibaraka tu hao, nia yao ni kuidhoofisha CHADEMA, jambo ambalo hawataliweza" Alisema Makene
Kwa upande wake katibu mkuu wa ACT,Samson Mwigamba alisema anaamini ipo orodha ndefu ya wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa ambao wako tayari kujiunga na chama chao ...
Mbali na Mwigamba, chama hicho pia kinaongozwa na Kadawi Limbu ( Mwenyekiti ),Ramadhani Ramadhan (Makamu mwenyekiti ) na Leopold Mahona ( Naibu Katibu mkuu )
3 comments:
Huu ni upuuzi wa hali ya juu kama hawa ACT wameamua kutoa habari, Inakuwaje wasitaje na majina na vyeo vya hao wanaowazungumzia..!!???
Kaaaaaazi kweli kweli
Political tactics!!!
Hahahaaa hawa ACT wana propaganda kwikwikwiii
Siasa ni kama brand name halikuwa over night
Post a Comment