ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 4, 2014

WAZANZIBAR WASEMA SERIKALI MBILI ZATOSHA


  • Wananchi wa Zanzibar wasema serikali mbili zatosha
  • Wachukizwa na wanasiasa wanafiki wanaopindisha pindisha maneno
  • Vijana wa CCM kutovumilia wanasiasa wanaokashifu waasisi wa Taifa letu
  • Wasema wamechoshwa na matendo ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani wataka muswada wa kuujadili Serikali wa Umoja wa kitaifa wataka ufutwe kwani hauna faida kwa maendeleo yao .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Zanzibar na kuwaambia CCM itasimamia haki za Wazanzibar na kuhakikisha Muungano unadumu na Mapinduzi ya Zanzibar yanaenziwa .
 Wananchi wakionyesha ishara ya Serikali mbili kwenye mkutano wa CCM kwenye viwanja vya Kibanda Maiti, Unguja Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto akionyesha ishara ya serikali mbili wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kibanda maiti na kuwataka wanawake wote wa Zanzibar kuungana katika kusimamia Muungano wa Tanzania.
 Mbili zatosha.

 Kila mtu alionyesha mapenzi yake kwa CCM.
 Wakazi wa Zanzibar hawakujali mvua iliyokuwa inanyesha kwenye mkutano wa CCM Kibanda Maiti Zanzibar
 Mama Fatma Karume akihutubia wakazi wa Unguja na kuwaambia kuwa waasisi wetu waliweka uzio wa kutulinda na kudumisha umoja na undugu wetu na kusema uzio huo ni Muungano wetu.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge wa BundaStephen Wassira akihutubia wananchi wa Zanzibar ambapo alisema UKAWA wanatakiwa kuelewa misingi ya Muungano kwanza kisha waje na hoja .

Mbunge wa Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibanda Maiti na kuwataka wananchi hao kuwa makini na viongozi wanaogeuza maneno huku akitolea mfano kutoka kwenye kitabu cha Maalim Seif.
Katibu wa NEC  Oganizeshen Dk. Mohamed Seif Khatibu akihutubia wakazi wa Unguja kwenye mkutano wa hadhara Kibanda maiti .

Sehemu ya Umati uliohudhuria mkutano wa hadhara ambao ulihutubiwa na Viongozi mbali mbali wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Makamu Mwenyekiti wa UWT Bi.Asha Bakari Makame akihutibia umati uliofurika kwenye viwanja vya Kibanda Maiti  na kuwaambia Wazanzibar wanaelewa maana ya Muungano na hawapo tayari kuuvunja kwa namna yeyote.
 Viongozi wa CCM wakifuatilia kwa makini hoja mbali mbali za kujenga na kuimarisha Muungano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa pamoja na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd (kushoto) Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Bunda CCM Ndugu Stephen Wassira ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Borafya Silima (kulia) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakifuatilia mkutano wa hadhara bila kujali mvua iliyokuwa inanyesha.

4 comments:

Anonymous said...

Ikiwa huu ndio umati wenu basi ni hasara kubwa sana. Gari bure, fulana bure, na mupo mjini na watu wakuhesabika. Hanna lenu Zanzibar tafuteni mganga haraka sana awajulishe mchawi wenu. Kikulacho kinguoni mwako CCM Zanzibar.

Anonymous said...

Hata c.u.f wanatoka kwao pemba wanakuja znz kwenye mikutano na gari bure, T.shirt bure na kofia bure....ili haki itendeke cuf wawe na serikali yao kama wakipata na ccm wawe na serikali yao hatutaki umoja wa kitaifa hauna maslah kwa wanaznz

Unknown said...

Inna Lilah wa Inna Ilaih Rajiun
Watizame sura zao zilivyo choka kwa uzalim walionao.
Rukeni mkitoja Wazanzibari hawana habari na mbili zenu mutabakia na matusi yenu tu mkumbuke tu mwisho wenu unakaribia.
Wasira jitizame kuanzia kichwani mwako hadi miguuni jee unahaiba yeyote ya kuwavutia Wazanzibari yaguju,
Asha Bakari tafuta tasbihi ustaghafiru kwa mola wako.
Nape siasa zako za matusi kazifanyie kwenu Tanganyika Wazanzibari unawatia kichefu chefu.
Moh'd Seif Khatibu naona viatu vyako vinaanza kukupita kimo umekwisha dalali wa Wazanzibari.
Wengine hamna jipya tupisheni.

Anonymous said...

wanahaha kama wamesomea halal badri wanajua sasa wazanzibari hawataki maskhara wanataka sherikali tatu na ccm ndo wanaotaka serikali mbili kwa sababu ya uchuu wao wa madaraka

na bado halal badri ya mbayana inawaumbua sasa watizame nyuso zao zimepigwa zimewachupa kama jiwe la kiyama

na bado mtahaha mliopata halal badri ya mbayana