ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 8, 2014

BAADA KUGOMEA DOLA LAKI 1 MASAA 12, CAMEROON WAKUBALI KURUKA KWENDA BRAZIL!


>>FIFA HUTOA DOLA 1.5 MILIONI KWA KILA NCHI KWA MATAYARISHO!
SAMUEL_ETOO_IN_CAMEROUN12BAADA KUGOMEA KWA MASAA 12 kupanda Ndege kwenda Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia wakipinga Bonasi hafifu, Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cameroun hatimae wamekubali kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Kikosi cha Cameroun, ambacho pia yumo aliekuwa Straika wa Chelsea, Samuel Eto'o, mmoja wa Wachezaji wenye Utajiri wa kutupwa, walikataa kusafiri mapema hii Leo wakidai Bonasi yao ni ndogo.
Lakini, baada ya Kikao cha Dharura na
Shirikisho la Soka la Cameroun, FECAFOOT, Wachezaji hao wamekubali kusafiri na wanategemewa kuondoka Mjini Yaounde, Cameroun Saa 5 na Nusu Usiku huu, Saa za Bongo, ikiwa ni uchelewesho wa Masaa 12 kupita ilivyopangwa.
Kocha wa Timu hiyo, Volker Finke, alidai Wachezaji walikuwa wakilalamikia kwamba £61,000 [Ni kama Dola 103,000] walizoahidiwa kulipwa kwa kuwepo tu Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ni ndogo.
Kwa mujibu wa FIFA, Kila Nchi ambayo inashiriki Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil hupata Dola Milioni 1.5 kwa ajili ya matayarisho yao.
Huko Brazil, Cameroun wapo KUNDI A pamoja na Brazil, Croatia na Mexico.
DONDOO MUHIMU ZA KOMBE LA DUNIA
ZAWADI
-Kila Nchi ambayo inashiriki Fainali hizi itapata Dola Milioni 1.5 kwa ajili ya matayarisho.
-$8 million – Kwa kila Timu itayotolewa Hatua ya Makundi (Timu 16)
-$9 million – Kwa kila Timu itayotolewa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 (Timu 8)
-$14 million – Kwa kila Timu itayotolewa Robo Fainali (Timu 4)
-$20 million – Timu itakayoshika Nafasi ya 4
-$22 million – Timu itakayoshika Nafasi ya 4
-$25 million – Mshindi wa Pili
-$35 million – Bingwa
KOMBE la DUNIA
RATIBA-Mechi za Ufunguzi:
[Saa za Bongo]
Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A
2300 Brazil v Croatia
Ijumaa 13 Juni 2014
1900 Mexico v Cameroun
KUNDI B
2200 Spain v Netherlands
0100 Chile v Australia
SOKAINBONGO

No comments: