Bebeto katikati katika staili yake ya ushangiliaji akiwa na Romario na Mazinho |
UNGEPENDA kukumbuka tukio lililofurahisha
wakati wa michuano ya kombe la Dunia lililofanyika Marekani mwaka 1994?
Moja ya tukio la kukumbukwa katika
fainali hizo ilikuwa aina ya ushangiliaji inayoelezwa kuwa ya kipindi chote
iliyoasisiwa na kiungo mshambuliaji wa Brazil, Bebeto.
Bebeto, katika medani ya soka, ndiye
anayeelezwa kuwa muasisi wa staili ya kuchezesha mikono kama amebeba mtoto wakati
akishangilia.
Alifanya hivyo baada ya kufunga goli la
kwanza la mchezo baina ya Brazil na Hollad; baada ya kufunga goli hilo Bebeto
alikimbia hadi karibu na kibendera na kusimama katikati ya Romario na Mazinho
ambao kwa pamoja waliiga staili hiyo ya ushangiliaji iliyokwenda sambamba na
furaha ya kuzaliwa kwa mtoto wake Mattheus Oliveira.
Mtoto huyo wa Bebeto hivi sasa anacheza
kikosi cha kwanza katika timu inayoshiriki ligi kuu ya Brazil ya Flamengo.
Mungu wangu toka kipindi hicho hatuoni kwamba nasi tumekula chumvi.?
Bebeto na Mattheus (pamoja na mtangazaji wa luninga wa Brazil Patricia Poeta) wamekutana pamoja na kutengeneza tangazo la kibiashara la aina hiyo ya ushangiliaji wakati fainali za kombe hilo mwaka huu zikitarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Brazil. 20 years... Where does the time go, eh?
franck Leonard
No comments:
Post a Comment