Mahakama ya juu nchini Libya
imesema kuwa kuchaguliwa kwa Ahmed Maiteg kama waziri mkuu mwezi
uliopita ulikiuka katiba ya taifa hilo.
Maiteeg aliyeapishwa kuwa Waziri mkuu mwezi uliopita na
bunge la taifa ,baada ya kura iliyokumbwa na utata.
Kuchaguliwa kwake na hatimaye
kuapishwa kuliipelekea taifa hilo linalosakamwa na vita vya wenyewe kwa
wenyewe tangu kung'olewa mamlakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo
Muammar Gaddafi ,kuwa na mawaziri wakuu wawili kwani waziri mkuu
aliyekuwepo Abdullah al-Thani alikataa kata kata kung'atuka mamlakani .
Maiteeg mwenye umri wa miaka 42 na anayetokea Misurata alichaguliwa baada ya kuungwa mkono na mirengo ya waislamu .
Hata hivyo taifa hilo limegawanyika kati ya waislamu wa kadri na wale wenye misingi kali ya dini.
Mirengo hiyo ya waislamu ndiyo yanayodhibiti maeneo tofauti ya Taifa hilo.
Uchaguzi unatarajiwa kufanyika terehe 25
June,kuchagua bunge la taifa litakalorithi nafasi inashikiliwa kwa sasa
na kongamano la kitaifa al maarufu '' General National Congress'
No comments:
Post a Comment