Naona
kuna watu wanahoji kwa nini siweki picha za misiba inayotokea ya ndugu
zetu wasanii wa Bongo Movie. Jibu ni kwamba maisha ni mipango na
maamuzi. Niliamua sitaweka picha za misiba katika mitandao ya kijamii
kwa sababu kiuhalisia hazisaidiii chochote kwa yule aliyetutoka na hata
faraja kwa ndugu, familia na marafiki zake.
Nachojua ni kwamba mambo
kama haya yanapotokea ni kumshukuru Mungu kwa yote, tena kwa faragha na
kutoka moyoni mwako na sio kumshukuru kwa kuposti mapicha
kwenye mitandao ya kijamii, tena wengine kwa kumdhalilisha hata
marehemu kwa kuposti picha zisizostahili. Kwa hiyo basi niwaombe woooote
mliokuwa mnasubiri niposti picha za misiba, siposti ng'oo! Kwanza hamna
shukrani.
Niliwahi kuposti mara moja na ya mwisho picha nikiwa kwenye
msiba wa Ngwea mkasema oooh anauza sura msibani. Sasa nimeacha kuposti
mnasema ooooh mbona hashiriki. Nyau kabisa! Na kwa taarifa yenu misiba
yote ambayo ilitokea nikiwepo nilihudhuria na ambayo sikuwepo nyumbani
nilitoa pole na kwenda kuwaona ndugu na familia za ndugu waliotutangulia
niliporudi. Sitaweka picha za aina hiyo hapa.
Hapa ni mwendo wa
makomedi, mastetasi, majoksi, n.k. Kama ulini-like ili uwe unapata picha
za msibani chapa mwendo. Eti oooh, kioo cha jamii (huku umebana pua),
kabla hujaniita kioo cha jamii kumbuka na mimi ni binadamu na nina
feelings na nasoma comments zenu na nina maamuzi yangu. Nimefinishi
mwanawane senki yu veri machi.
1 comment:
Mwanawane hao hawana hofu ya mungu wala hawakumbuki maneno yasemayo
Msitake kujuwa habari za waliyo lala mauti juweni habari zenu
Post a Comment