ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 9, 2014

DK SHEIN AFUTARISHA WANANCHI WA PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) akiwakaribisha Mashekhe katika futari aliyoiandaa kwa Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba huko Viwanja vya Ikulu ya Wete jana.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. 
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na akinamama na Viongozi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana. 
Baadhi ya akinamama mbali mbali wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari aliyowandalia na Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba jana. 
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (aliyesimama) alipokuwa akitoa shukurani pamoja na kuomba dua baada ya kumaliza kufutari wananchi waumini wa Dini ya kiislamu,futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba jana. 
Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete ,
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiagana na akinamama mbali mbali na Viongozi waliohudhuria katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba jana. 

[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

No comments: