Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula (kushoto) akisaidiana na Meneja wa Kampuni ya utengenezaji wa vinywaji baridi vya Pepsi Mwanza, Nicolas Coertz wakikagua utaratibu wa zawadi pamoja na vitendea kazi vya michuano ya Pepsi kombe la meya 2014 kabla ya kuvikabidhi kwa viongozi wa timu 22 zitakazo shiriki michuano hiyo.
Balozi wa Habari wa Pepsi Kombe la Meya 2014, G. Sengo akitoa utaratibu utakao fuatwa kabla ya makabidhiano.
Mstahiki Meya aliiongoza meza kuu.
Timu yenye nidhamu itaondoka na kitita cha shilingi laki mbili.
Zawadi ya refa bora wa mashindano shilingi laki mbili, ile hali mshindi wa tatu atalitwaa kombe, medali ya shaba na kitita cha shilingi milioni moja.
Ni makombe na medali zake kwa michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014.
Uchapishaji kwa zawadi ya mshindi wa kwanza (kushoto) ulikosewa ni shilingi milioni moja na nusu (1500,000/=) ndizo atakazo ondoka nazo bingwa wa Pepsi Kombe la Meya 2014 ambapo mbali na kitita hicho pia bingwa huyo atakabidhiwa Kombe, medali ya dhahabu na bajaji ya kisasa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba pia watu wanne yenye thamani ya shilingi milioni 4.5, huku mshindi wa pili wa michuano hiyo akiondoka na kombe, medali ya fedha na kitita cha shilingi milioni mbili.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kulia) akiwa na Meneja wa Kampuni ya Kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi ya Pepsi wakipongezana mara baada ya kumaliza zoezi la kukagua vifaa kabla ya kuvikabidhi kwa timu 22 zitakazo shiriki Michuano ya Pepsi Kombe la Meya 2014.
Team Pepsi. Picha kwa hisani ya Gsengo Blog
No comments:
Post a Comment