ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 21, 2014

MILA ZA MIKOA YA KUSINI, LINDI, MTWARA JITIRIRISHE HAPA CHINI

Jando ni sheria na mila za watu wa mikoa ya kusini mtoto wakiume anavyotimiza umri wa miaka 7 upelekwa jando kwa mafunzo ya jinsi ya kuwa na nidhamu kwa watu wazima waliwazidi kimri. Mafunzo hayo huendana sambamba na kutahiriwa na kisha kupelekwa msituni kuishi kwa mafunzo hayo. Pia watoto wakike upata mafunzo kama hayo baada ya wiki kupita tokea watoto wakiume wapelekwe msituni, lakini mafunzo ya watoto wa kike ufanyika nyumbani sehemu ambayo wanaume awaruhusiwi kuwaona. Watoto wa kike ni tofauti kwani hupewa mafunzo tu bila kutahiriwa kama wanaume. Mafunzo hayo uchukua wiki 3 hadi 4 na kisha hutolewa kwa kufanyiwa sherehe sambamba na kuvalishwa nguo mpya.
Watoto wakiwa na nguo mpya baada ya kufanyiwa sherehe ya kurudi nyumbani baada ya kupokea mafunzo ya jinsi ya kuwa na nidhamu kwa watu waliowazidi kimri.
(Jando na unyago)
Hii ni sehemu ambayo  watoto wakiume walifichwa wakipokea mafunzo huko msituni inavyofika siku ya mwisho huchomwa moto na wazazi wawatoto hufika kwa mara ya kwanza na kuzunguka sehemu hiyo wakiimba na kupiga vigelegele kama furaha ya kuwaona watoto wao salama. Kwani wakiwa huko msituni wanaume tu ndiyo wanaoruhusiwa kuwatembelea.
Hapa nyumba hiyo ikianza kuwaka moto akina mama wakianza kuizunguka kwa mbio na nyimbo
Jamaa akiwa kazini akipiga ngoma kwenye sherehe hizo za jando kwa wale waliotoka mikoa ya kusini hii inawahusu na kuwakumbusha kuwa nyumbani ni nyumbani. Shughuri hizi za jando ufanyika kipindi cha likizo za kiangazi watoto wakifunga shule ili wakimalizana na mafunzo hayo wanarudi shule kuendelea na elimu.

1 comment:

Anonymous said...

Mambo yamebadilika zamanijandoni walipelekwa watoto wakubwa wenye uwezo wa kushika mafundisho tofauti na sasa. hata hivyo inasaidia kidogo mtoto kujielewa na kuwa na nidhamu. Imenikumbusha zamani sana Ntengu na Chiputu