Kufuatia sakata la Flora Mbasha na mumewe likumuhusisha moja moja kiongozi wa kiroho Mchungaji Gwajima, habari tulizozipata ni kwamba mchungaji huyo amekimbia nchi….
Habari toka chanzo cha kuaminika kilichopo ndani ya kanisa la mchungaji huyo ni kuwa Gwajima hivi sasa ameshauza karibia robo tatu ya mali zake na kwamba moja kati ya magari yake ya kifahari huenda likanunuliwa na mwanamuziki Diamond.
“Jamaa hivi tunavyoongea anaweza akawa ameshatoroka tayari, maana hili sakata limeanza kumwendea hovyo na wiki iliyopita kuna madalali walikuja hapa wakiitaka gari yake aina ya Hammer, wakidai kuwa inataka kununuliwa na mwanamuziki Diamond,” kilisema chanzo cha habari hii.
Kikaendelea kumwaga data kuwa karibu wiki zima lililopita mchungaji huyo alikuwa kwenye mipango ya kuuza baadhi ya nyumba zake na kwamba hata familia yake hivi sasa haiko kwenye makazi yake anayoishi siku zote…
“Hata familia yake sijaiona karibu wiki mbili hapa kanisani na taarifa tulizonazo karibu waumini wengi tu ni kwamba jamaa anataka kuhama nchi lakini hatujui ni nchi gani anayotaka kwenda kufanya makazi yake tena ya kudumu,” alisema.
Habari hizo zinadai kuwa baadhi ya waumini wamepanga kugawana mali kadhaa za kanisa pamoja na za Gwajima mwenyewe endapo itagundukia kuwa ametoroka kweli….
2 comments:
Sisi ni nani hata tuwahukumu watumishi wa mungu.
HAPA SI KUHUKUMU BALI APANDACHO MTU NDICHO ATAKIVUNA. GWAJIMA NI MTU KAMA WANADAMU WENGINE, ANAMAPUNGUFU KAMA WENGINE, HIVYO ILIMBIDI AJIEPUSHE NA ZINAA KAMA BIBLIA ISEMAVYO. KAMA HAKUFANYA HAYO KWANINI AKIMBIE? HUKUMU YA MUNGU ITAMFUATA HUKO HUKO....ZABURI 139:5-13. KUHUBIRI SI UTAKATIFU BALI UTAKATIFU NI KUIKATAA DHAMBI NA KUSHIKAMANA NA MUNGU KTK KWELI YOTE
Post a Comment