Na Liberatus Mwangombe “Libe”
TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014
Ijumaa July 18, 2014 tulikuwa na mkutano kwenye ubalozi wa Tanzania Wshington D. C. ulio tuhusisha wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jumuia ya DMV, viongozi wa Tume ya Uchaguzi, ATC Metro Board members na kusimamiwa na balozi Liberata Mulamula. Kwenye mkutano huu wagombea tulitoa malalamiko ya jinsi uchaguzi umekuwa ukiendeshwa bila haki na sintofahamu lote linalo uzunguka uchaguzi huu.
Kikao kilifunguliwa na Mh. Balozi, Mulamula, ambapo aliweka misingi ya kikao kuwa ni kutafuta maridhiano, amani na upendo hapa DMV. Huku akiendelea kutoa utangulizi, Mh. Balozi Mulamula aliweka wazi kuwa tarehe ya uchaguzi haiwezi kubadirishwa; mimi binafsi nilitafsiri msimamo huu kuwa balozi amesha fanya maamuzi bila kutushirikisha, ilihali, hili ni moja ya tatizo ambalo tulitaka ufumbuzi wake. Pia niliendelea kujiuliza yeye, balozi, anafanya maamuzi haya bila muafaka kama nani! Baada ya kufungua kikao, mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi Ndg. Safari aliongea machache kuhusu mchakato wa uchaguzi huu na kazi ngumu ambayo tume ya Uchaguzi inapitia. Baada ya hapo, Mama Salma Manyoka/ mgombea makamu wa Rais aliongea yafuatayo
Mama Salma Manyoka
Mimi kama mgombea ninasikitika namna Tume ya Uchaguzi inavyo fanya kazi; Tume imekuwa ikifanya maamuzi bila kutushirikisha na kutushutukiza. Hadi hivi sasa hatuja wahi kuwa na mkutano na Tume. Kwa ufupi Mama Salma aliweka pingamizi la badiriko la tarehe ya uchaguzi ya August 9, 2014. Aliomba tarehe isogezwe mbele.
Nilifuatia mimi, Liberatus Mwang’ombe, mgombea wa nafasi ya Urais. Nilieleza jinsi baadhi ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wanavyo vunja maadili ya Tume na kukiuka haki. Binafsi nilieleza namna Asha Nyang’anyi alivyo vunja maadili ya Tume ya Uchaguzi na kumfanyia kampeni Ndg. Idd Sandaly. Kwa hili nilienda na vithibitisho ambavyo nilivionyesha kwenye kikao. Nilionyesha email zaidi ya sita ambazo Ms. Nyang’anyi alikuwa akinitumia mimi na kupinga yale niliyo ongea kwenye mkutano wa kampeni wa June 28th 2014. Kwenye mzunguko wa email hizi kulikuwa kuna watu watano wapo cc’d, ambao ni Raymond Abraham, Amos Cherehan, Bernadeta Kaiza na Idd Sandaly ambaye tunawania Urais wa DMV wote. Niliweza kuonyesha namna Ms. Nyang’anyi alivyo kiuka maadili ya Tume ya Uchaguzi na kusema sina imani naye tena.
Hoja yangu iliongezewa uzito na ushahidi nilio upeleka pale wa email mbili za Ndg. Cherehani ambaye alimwambia Ndg. Asha kuwa, “suala la mgombea kutumia kipindi hiki ambacho darasa limefungwa kutafutia kura mimi silioni kama ni tatizo maana mwisho wake ni kuijenga jumuia yetu ili iwe bora zaidi na pia kuja na ideas ambazo zitalifanya darasa letu liwe bora zaidi”. Ndg. Cherehani akaongeza “ Ms. Nyang’anyi, kutokana na nafasi yako uliyo nayo sasa kwenye Tume ya Uchaguzi, mie nashauri ukae kando katika hili maana linatafsiriwa kama tume inaipigia kampeni Jumuia na viongozi walioko madarakani jambo ambalo nadhani linaleta mkanganyiko wa kimaslai.” Ms. Nyang’anyi hakusikia maoni haya na kuendelea kuni “harrass” na emails.
Baada ya email hii ya Ndg. Cherehani kumshauri Ndg. Asha kuto kuendelea ku “intervine” kampeni zangu; Ndg Asha, Idd Sandaly, Raymond Abraham waliendelea kuni “harrass” kwa kunitumia email ambazo zilizidi kumi ndani ya siku moja. Mimi sikujibu hata email moja. Nilicho kifanya ni kutuma email kwenye Bodi na Tume ya Uchaguzi kuwa nimekuwa harrassed na mjumbe wa Tume ya Uchaguzi na naomba aache kufanya hivyo haraka. Sikujibiwa na Bodi wala Tume ya uchaguzi; na Ms. Nyang’anyi aliendelea kunitumia email siku ile.
Huku nikiendelea kushambuliwa na email kutoka kwa Raymond, Asha, na Idd; Ndg. Cherehani aliandika email ambayo ilikuwa ni ya mwisho na hakuandika tena. Sehemu ya email hiyo ilisisitizia Ms. Nyang’anyi kuharibu maadili ya Tume ya Uchaguzi, nanukuu email ya Cherehani ya pili “Bado mimi nipo palepale kwenye ushauri nilioutoa hapo awali kuwa ili kuepuka conflict of interest, Ms. Nyang’anyi kwa nafasi uliyo nayo, ungewaachia viongozi wa jumuia wakalizungumzia hili na hata President Sandaly kwani analijua darasa la Kiswahili tangu mwanzo hadi mwisho”.
Baada ya kutoa maelezo jinsi mjumbe wa tume ya Uchaguzi kuvunja miiko ya Tume nilielezea swala lingine kuu la ubadirishwaji wa tarehe ya uchaguzi bila kutaarifiwa wala kushirikishwa. Nilieleza kuwa mimi kama mgombea sikutaarifiwa mabadiliko ya tarehe na nilitumiwa email kuwa uchaguzi utakuwa Augus 2, 2014; ndani ya masaa 24 niliona tangazo kwenye blog ya Vijimambo likisema uchaguzi ni August 9, 2014. Niliandika email haraka na kusema kuwa nimechanganyikiwa kwa kuwa na tarhehe mbili za uchaguzi; pia niliandika email ya kupinga mabadiliko hayo. Sikujibiwa hadi leo! Kwenye mkutano huu nilieleza umuhimu wa kusogeza tarehe ya uchaguzi mbele kwa kulingana na madai ya wana jumuia wengi wakiwa likizo ya “summer”. Hoja hii iliungwa mkono na wagombea wanne, mimi, Ismail Mwilima, Salma Moshi na Solomn Cris. Cha kusikitisha hoja hii ilipuuziwa na Balozi alikuwa amesha weka msimamo mwanzo kuwa tarehe ya uchaguzi haitabadirishwa. Kauli hii ilijirudia mara kwa mara kuwa “tarehe ya uchaguzi haitabadirishwa”; kauli hii ilitukera wengi na kuna wakati Ndg. Ismail Mwilima mgombea wa nafasi ya Ukatibu aliongea kwa sauti kuwa “HATUTAKI KUBULUZWA”. Ismail aliongeza kuwa tunafanya kikao hiki kwaajili ya maridhiano na sio kukandamizana.
Solomon Cris
Baada ya Ismail kumaliza kuongea, alipata fursa Ndg. Solomon Cris ambaye alikuwa ana malalamiko na Asha Nyang’anyi. Malalamiko ya Solomon yalikuwa ni njama za kutaka kumkomoa yeye na kumuwekea mgombea mwenza ilihari muda wa kuchukua fomu uliisha. Solomon alieleza kuwa njama hizo zilianzishwa na Ndg. Idd Sandaly ambaye aliiamuru tume imuwekee Solomn mpinzani. Solomon alikuwa na ushahidi wa maandishi wa kauili ya Ndg. Idd Sandaly. Aliumwaga ushahidi hazarani. Pia alieleza namna Ndg. Nyang’anyi anavyo kiuka maadili ya uchaguzi kwa kumfanyia kampeni Ndg. Idd Sandaly. Baada ya maelezo yake na ushahidi Ndg. Solomon aliomba Ms. Nyang’anyi ajiuuzuru kwa kuwa amekiuka miiko ya Tume ya Uchaguzi na yeye na mimi, Libe, hatuna imani naye tena. Hoja hii ya kuomba Ms. Nyang’anyi ajiuzuru ilifumbiwa macho na kutakiwa tume iombe msamaha.
Baada ya swala la Ndg. Asha Nyang’anyi kumalizika na kuthibitika pasi na shaka kuwa amekuwa akikiuka maadili ya Tume ya Uchaguzi; hoja hiyo ilitupiwa kapuni na kuendelea na hoja nyingine. Hoja nyingine iliyo jadiliwa ni ya “absent ballot” ambayo ilipata pingamizi kutoka kwa baadhi ya wajumbe na kusema inaweza sababisha “fraud”. Mimi binafsi niliona umuhimu wa wanaDMV ambao hawatakuwepo hapa na ni wanachama hai wafikiriwe kwa kushiri uchaguzi kwa “absent ballot”. Hoja hii haikupata muafaka na tunasubiri neno kutoka tume ya uchaguzi.
Huku kikao kikiendelea mgombea wa makamo wa Rais Bi. Heriet Shangarai aliomba kuongea na kusema yeye anajitoa kwenye kugombea kwa sababu hawezi ku “deal” na haya mambo kwani yeye kipaumbele chake cha kwanza ni kusaidia na sio kufanya mashindano yasio na maana. Baada ya hapo tulipata mapumziko ya kufuturu. Asante ubalozi kwa kutuandalia futari. Tulivyo rudi baada ya futari Ms. Shangarai alisema hawezi kuendelea kukaa pale kwani ana dharura. Aliondoka.
Ngwe ya pili ikiendlea Ndg. Ismail Mwilima alibadirisha msimamo wake wa kukataa uchaguzi usifamnyike august 9, 2014 na kuikubali hiyo tarehe. Katika hoja zake za awali Ndg. Mwilima alisema kuwa Tume haikuwasiliana/kumshirikisha na yeye wakati inafanya mabadiriko ya tarehe; na Agust 9, 2014 atakua nje ya nchi. Nilishangazwa na Ndg. Ismail kubadirisha msimamo! Baada ya kikao Ndg. Solomon aliniambia kuwa alimuona balozi akimpa kimemo Ismail wakati mkutano ukiendelea kwenye ngwe ya pili. Tulipo muuliza Isamail baada ya kikao kuwa kile ki memo kutoka kwa balozi kilikuwa cha nini; alikili kuwa balozi alimuomba abadirishe msimamo ili mambo yaishe. Hadi tunaondoka kwenye kikao mimi, Liberatus, mama Salma na Solomon hatukuridhia uchaguzi ufanyike August 9, 2014. Binafsi hadi sasa nipo kwenye tafakuri jadidi la kuangalia hatua nyingine, nitawajurisha baada ya kuongea na washauri na Team kampeni yangu.
Zaidi ya haya, mimi kama mgombea na mwanachama hai wa jumuia nilifikisha malalamiko kuwa niliomba “records” za jumuia, lakini Board, Tume ya Uchaguzi, na Tresury wa jumuia hawaja nijibu hadi leo. Nilifikisha barua hiyo kwenye kikao hiki. Cha kushangaza Ndg. Idd Sandaly alisema hawezi kutoa “records” za jumuia kwani mimi ninataka kuzitumia kwenye kampeni kumkandamiza yeye. Nilijieleza kuwa nina haki ya kupata hizo records na hakuna kipengele kwenye katiba kinacho nizuia; ninacho takiwa ni kuwa mwanachama hai. Niliomba record ya mambo mengi. Kama msomaji unataka kuyajua, tafadhari niandikie email au nipigie simu. Ilitoka amri kuwa siwezi kupata hizo record isipo kuwa nitapata “financial statement za 2012, 2014 and year to date”. Nilijaribu kuuliza hizi record zitakuwa tayari lini kwaajili ya kuzichukua au kutumiwa kwenye email; hakukuwa na jimu stahiki.
Hitimisho
Binafsi kikao hakikuwa na manufaa kwangu kwani madai mengi ya kimsingi yalifumbiwa macho, mfano, moja; kumuomba Ndg. Nyang’anyi ajiuzuru kwa kukiuka maadili ya Tume ya Uchaguzi, mbili; balozi kuweka msimamo wa kutobadirisha tarehe ya uchaguzi ilihari tulienda pale kwaajili ya maridhiano na hili ni tatizo mojawapo ambalo wagombea wanne tuliipinga hiyo tarehe mpya yaani August 9, 2014. Pia, mimi binafsi kunyimwa baadhi ya kumbukumbu za jumuia huku Ndg. Idd Sandaly akisema nataka kuzitumia hizo kumbukumbu kumkandamiza yeye kwenye kampeni. Bado nashangaa ni nini Ndg. Idd Sandaly anajaribu kuficha wakati kumbukumbu za jumuia ni huru kwa kila mwana jumuia! Mwisho, kama Mh. Balozi anasoma walaka huu; naomba atumie busara za ziada kuitisha kikao kingine haraka na kurekebisha haya niliyo yaweka kwenye walaka huu. Kwa kifupi; UCHAGUZI HUU UNAENDESHWA KINYUME NA SHERIZIA ZA KATIBA YA JUMUIA NA MAADILI YA UCHAGUZI.
UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL
TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014