ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 6, 2014

LINA SANGA MWANZA

Balozi wa wanawake mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Linah Sanga (katikati) akiwa na warembo wa kinyang'anyiro cha Redds.Linah Sanga akimsaidia mmoja kati ya mama lishe wa eneo la Kamanga Ferry kuhudimia wateja.
Linah Sanga akinunua samaki kwa mama Veronica Chalo ambaye ni mfanyabiasha.
Linah akizungumza na mama mfanyabiashara wa vitunguu mama Lenest.

Na Mashaka Baltazar,MWANZA

MSANII wa Kizazi Kipya, Linah Sanga amewataka akina mama wajasiriamali kutokatishwa tamaa na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye shughuli zao za utafutaji.

Pia amewaasa wawe wabunifu na kuwa wadadisi kwa wengine waliofanikiwa ili waweze kufanikiwa katika kazi zao.

Linah ambaye aliwasili Jijini Mwanza jana kwa ndege ya Air Precision majira ya saa 4:00 asubuhi, alitembelea wajasiriamali wa soko la kimataifa la Kirumba Mwaloni na eneo la Kamanga Ferry,ambapo alipata fursa ya kuzungumza nao na kubadilishana mawazo .

Akizungumza kwa nyakati tofauti Linah alisema, akiwa Balozi wa wanawake,akina mama wajasiriamali na akina dada,amekuja jijini hapa kuwatia moyo ili wapambane na changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za ujasiriamali.

Alisema changamoto hizo ni sehemu ya maisha, hivyo zisiwe kikwazo cha kuwakatisha tamaa katika utafutaji,kwani hata yeye katika sanaa ya muziki alikumbana nazo akazivuka pamoja na vikwazo vyake.

Alidai juhudi zake na kutokata tamaa zilimfanya aonekane ndani ya kundi la wasanii wenye uwezo zaidi yake,hivyo juhudi,maarifa,kujituma na ubunifu, ndiyo njia pekee itakayowasaidia kufikia mafanikio ya malengo yao.

Aliwataka wajasiriamali hao wajitume zaidi katika biashara zao na waonyeshe ukaribu kwa wateja ili wapate mafanikio,huku wakijaribu kuonyesha jinsi wanavyoheshimu kazi zao kwa kuwaonyesha watu kuwa hizo ndizo kazi zao,bila hivyo hawawezi kufanikiwa.

“Nikiwa Balozi wa wanawake,nimekuja hapa kuwatia moyo dada zangu na akina mama wajasiriamali.Lengo kubwa likiwa ni kuwabadilisha fikra,sababu siku zote wako nyuma kwa kutokubali kubadilika.Wanafanya kazi kwa kukariri bila kujituma na kutazma wengine kwa nini wamefanikiwa,”alisema Linah

Alisema wengi wa wajasiriamali hawajiulizi kwamba wanaweza,pia hawaulizi kwa nini yeye ameweza , ni kwa sababu aliweza kupigana na kufanikiwa.

Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya,alipata mapokerzi makubwa akianzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwanza,ambapo alipiga picha kwenye vivutio vya utalii vya jiji la Mwanza alivyotembelea vya miamba ya mawe ya Bissmark, sanamu ya samaki kabla ya kuelekea Malaika Beach resort.

No comments: