Msafara wa Magari ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga ukiwasili katika Banda la Jeshi la Magereza katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi leo Agosti 7, 2014.
Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro akimkaribisha Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Raphael Muhuga alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi hilo katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Raphael Muhuga akisaini katika Kitabu cha Wageni katika Banda la Jeshi la Magereza kabla ya kutembelea sehemu mbalimbali za Banda hilo katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro.
Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(kulia) akimuongoza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Raphael Muhuga kutembelea sehemu mbalimbali za Banda hilo alipotembelea leo Agosti 7, 2014 katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa yanayofanyika Mkoani Lindi.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Raphael Muhuga akiangalia mazao mbalimbali ya Kilimo katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Agosti 7, 2014 katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, Mkoani Lindi(kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Raphael Muhuga akisikiliza maelezo ya Kitaalam kutoka kwa Mtaalam wa Mifugo wa Jeshi la Magereza(aliyeko kushoto) namna Uhamilishaji wa Mifugo unavyofanyika ili kupata Mifugo Bora na wa Kisasa zaidi katika Ufugaji wa Biashara na unaozingatia Matokeo Makubwa(wa Pili kulia) ni Mkuu wa Banda la Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Mlasani Kimaro(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment