ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 13, 2014

KINANA AANZA ZIARA KWA KISHINDO.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi pamoja na wananchi waliokuja kumpokea alipowasili Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga Adam Malima akisoma taarifa yake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye kikao cha halmashauri ya mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu akiendesha kikao cha halmashauri ya mkoa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Mwarusembe wilayani Mkuranga.
Wananchi wakishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Mwarusamba.
Wananchi wakijaribu kutafuta sehemu nzuri ya kukaa ili wamsikilize Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana.
Katibu wa CCM mkoa wa Pwani Joyce Masunga akiwatambulisha wageni walioongozana kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Mbunge wa Viti Maalum na ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Pwani Zainabu Vulu akisalimia wananchi wa Kimanzichana waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kimanzichana kwenye viwanja vya CCM Kimanzichana Kusini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kimanzichana ambapo aliwataka Viongozi kuchukua majukumu wanayoyaweza na si kujijazia vyeo ambavyo hawavimudu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana wa Kimasai wanaoishi Kimanzichana.

No comments: