ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 14, 2014

SHUKRANI NYINGI

Padri Evod Shao.

Ndugu zangu wapendwa,
Naomba nianze kwa kutumia maneno ya Mzaburi:-"Nikushukuruje Mungu wangu kwa wema wako kwangu, Nitakuchukua kikombe na wokovu na kukutolea sadaka ya Shukrani".
Ni mema mengi nimetendewa nanyi tangu nifike Marekani miaka ipatayo 9 hivi. Na Jumapili ya tarehe 31/9/2014 mlitenda wema usiopimika. Kuja kwenu kushiriki Misa takatifu kumkaribisha Padri Honest Munishi na kuniombea mema kwa safari iliyo mbele yangu nakosa hata maneno yanayofaa kutoa Shukrani zangu. Kwa kuwalisha umati ule wote uliofika kwa chakula bora! Asanteni Mno. Kwa zawadi mlizonipa Mungu awazidishie Baraka zake na kujazia pale mlipotoa mema mengi zaidi.
Nitawakumbuka daima katika maisha yangu na katika sala nitatolea nia zenu njema daima kwa Mungu. Mungu anajua kile kilicho chema zaidi kwa maisha yenu na awakirimie kwa fadhili zake.
Nategemea kuwa likizoni Tanzania hadi Januari 2015. Kwa kipindi hicho mawasiliano ya E-mail na Viber au Skype najua yatakuwa Rahisi. Kwa sasa sina Namba ya Simu ya Tanzania. Nikifika nitawajulisha.
Kunzia January nategemea kuwa California Berkley kwa kucharge bateri kidogo hadi Julai. Hapo nitakuwa nimejua wazi ni utume gani nitakaopangiwa.
Tafadhali popote pale nitakapokuwa, ikiwa utafika upande huo tuwasiliane na nitafurahi sana nikiweza kuwa mwenyeji wako.
Hapa chini ni kiunganishi kuweza kuona tulivyomeremeta siku ile.


Tuombeane daima. 
Wenu mwenye wingi wa shukrani
Pd. Shao

No comments: