Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira imeendelea na
ukaguzi katika Migodi ya dhahabu kufahamu utekelezaji wa Sheri a ya Mazingira.
Katika Mgodi wa Bulyanhulu Kamati iliangalia jinsi maji yenye kemikali
yanavyohifadhiwa na udhibiti wa taka za plastiki mgodini hapo. Migodi iliyotembelewa mpaka sasa ni
Mgodi wa North Mara, Geita na Bulyanhulu. Hii leo Kamati hii itaendelea na
ziara yake katika mgodi wa Buzwagi.
Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi wa
kisheria mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira. Kamati hiyo
iko katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Sheria ya Mazingira katika
Migodi. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mh. James Lembeli
(wa tatu kulia), Mh. John Mnyika na Mh. Henry Shekifu wajumbe wa Kamati hiyo.
Wa kwanza (kushoto) ni Bw. Peter Burger, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu.
Pichani ni taka za
plastiki zilizohifadhiwa vizuri kwa ajili ya urejelezwaji katika Mgodi wa
Bulyanhulu.
Wajumbe wa kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na
Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu wakati wa ukaguzi katika Mgodi huo kuona
utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
Wajumbe wa kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na
Watendaji wa Mgodi wa Bulyanhulu mara baada ya ukaguzi katika Mgodi huo kuona
utelekezaji wa Sheria ya Mazingira.
No comments:
Post a Comment