ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 29, 2014

Kina Halima Mdee wapigwa mabomu

Mbunge wa Kawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema (Bawacha),Halima Mdee.

Mkutano wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), uliopangwa kufanyika jana wilayani Kelwa mkoani Kagera, ulivurugika baada ya Jeshi la Polisi kupiga mabomu ya machozi kuuzuia.

Mwenyekiti wa Chadema, wa wilaya hiyo, Deus Lutakyamilwa, alisema Bawacha waliomba kibali cha kufanya mikutano katika wilaya hiyo Oktoba jana bila kujibiwa na polisi.

Alisema mabomu hayo yalipigwa juzi usiku katika kijiji cha Isingiro wilayani humo baada ya Bawacha kupinga agizo la mkuu wa polisi wa wilaya hiyo likiwataka kutofanya mkutano wowote katika wilaya hiyo.

Alisema, taarifa hizo za polisi zilitoka katika ngazi za juu.

Kwa mujibu wa Lutakyamilwa, walikubaliana na polisi kuwa baada ya wanawake kufika hawatafanya mkutano bali watasaini kitabu na kuwachukua wanawake wengine waliokuwa wakisubiriana kwa ajili ya mkutano wa ndani.

Alisema baada ya viongozi wa Bawacha kufika na kusaini kitabu katika ofisi za Chadema wilayani hapo walipanda gari kwa ajili ya kuelekea katika ukumbi waliokuwa wamepanga kufanyia kikao cha ndani, lakini ghafla polisi walifika na kuanza kupiga mabomu ya machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kuongozana na viongozi wa Bavicha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alipotafutwa jana simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

Anonymous said...

Tanzania haitakaa ibadilike, TERRIBLE COUNTRY, uonevu.com