Mkaguzi Mkuu Msaidizi kutoka Ofisi ya CAG,Benja Majura.
Hesabu za mapato na matumizi ya fedha za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa vyama vya siasa nchini, ikiwamo CCM, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, kati ya mwaka 2009 na 2013 zimegubikwa na dosari na hivyo kusababisha baadhi kupata hati yenye shaka na vingine hati mbaya kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Vyama vilivyopata hati zenye shaka kufuatia ukaguzi wa hesabu zake uliofanywa na CAG ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP na Chaumma.
Vilivyopata hati mbaya ni UMD, ADC, APPT-Maendeleo na NRA, huku ofisi ya CAG ikishindwa kuzitolea maoni hesabu za NLD kutokana na kutokidhi vigezo na UDP kutopeleka kabisa hesabu zake kwa CAG hadi sasa ili zikakaguliwe.
Mkaguzi Mkuu Msaidizi kutoka Ofisi ya CAG, Benja Majura, alisema hayo katika kikao kati ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, katika ofisi ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam jana.
Akijibu swali la Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, kuhusu maana ya hati yenye shaka, Majura alisema ni kuwapo upungufu au dosari zinazotakiwa zirekebishwe katika hesabu za chama husika.
Alisema tatizo hilo linatokana na kutokuwapo na wataalamu wa masuala ya uhasibu na pia kutozingatiwa kwa sheria ya manunuzi katika matumizi ya fedha za ruzuku ya serikali.
Awali, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, alisema kati ya vyama tisa, ambavyo hesabu zake zimekaguliwa, sita tayari vimeshawasilisha ripoti zake katika ofisi yake.
Vyama hivyo ni CCM, CUF, UMD, NLD, APPT-Maendeleo na ADC. Alisema vyama vitatu, ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi na TLP, licha ya hesabu zao kukaguliwa, hadi kufikia jana vilikuwa havijawasilisha ripoti katika ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema muda wa mwisho wa kuwasilisha ripoti hizo ni Oktoba 31, mwaka huu.
Alisema baada ya tarehe hiyo, hatua itakayofuata ni ofisi yake kutangaza kwenye Gazeti la Serikali taarifa ya vyama vilivyowasilisha ripoti zake.
Baada ya maelezo hayo, Zitto alimtaka Jaji Mutungi kueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya vyama ambavyo havijapeleka hesabu zake kukaguliwa na CAG.
Akijibu, Jaji Mutungi alisema kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa kifungu cha 18 (4) na (5), vyama vya aina hiyo vinaingia katika kundi la vyama vinavyotumia vibaya fedha za serikali.
Akifafanua, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, alisema sheria hiyo inampa mamlaka msajili kuvikatia fedha za ruzuku vyama vya aina hiyo katika mwaka unaofuata.
Nyahoza alisema pia kama msajili atabaini vyama hivyo vimeshindwa kuwasilisha hesabu zake kwa CAG, sheria inampa mamlaka ya kulikabidhi Jeshi la Polisi suala hilo.
Jaji Mutungi alisema kaguzi za hesabu za vyama vya siasa zinatoa picha kwamba, baadhi ya vyama havijajipanga kupokea fedha kutoka serikalini.
Kutokana na hali hiyo, alisema inawezekana ukafika wakati sheria ikarekebishwa na baadhi ya vyama vikakosa ruzuku.
Pia alisema hatua nyingine za kijinai zitafuata iwapo itabainika kuwapo na chama kilichohusika na makosa ya jinai katika matumizi ya ruzuku ya serikali.
Akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, kwamba kama ukaguzi unaweza kufanyika kwenye hesabu za fedha, ambazo chama kinapata kutoka kwa vyama marafiki, Jaji Mutungi alisema sheria inampa mamlaka CAG kukagua hesabu zote za vyama vya siasa bila kujali ni za serikali au watu binafsi.
Mkaguzi Mkuu Msaidizi kutoka ofisi ya CAG, Majura akizungumzia changamoto ambazo wakaguzi wanakumbana nazo katika kukagua hesabu za vyama vya siasa, alisema ni pamoja na baadhi ya vyama kutokuwa na mwongozo wa kuandaa hesabu, wataalamu na akaunti katika mabenki.
Pia ofisi za baadhi ya vyama vya siasa kupatikana mahotelini, kwenye makontena, vichochoroni, pia ofisi nyingine kuwa na kiti na dawati moja pekee na kuwa na karatasi moja iliyoandaliwa hesabu.
Zitto aliiagiza ofisi ya CAG, Msajili wa Vyama vya Siasa na wabunge kwenda nje ya nchi, kama vile nchini India, kujifunza uzoefu wa ukaguzi wa hesabu.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Faida Mohamed Bakar, alisema changamoto zinazovikabili baadhi ya vyama vilivyotajwa na ofisi ya CAG inachangiwa na kutopata ruzuku na kuhoji kwanini vyama hivyo visipewe ruzuku ili kuvisaidia kuendesha shughuli zake.
Akijibu, Jaji Mutungi alisema ofisi yake inafanya utafiti utakaoshirikisha ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuhusiana na suala hilo na kwamba, kuna uwezekano vyama hivyo vikawa vinapata asilimia 20 ya ruzuku na asilimia 80 ikaenda kwa vyama vyote vilivyopo kwenye utaratibu wa kawaida wa kupata ruzuku.
Hata hivyo, Mbunge wa Kibiti (CCM), Abdul Marombwa, alitahadharisha kuwa iwapo kila chama kitapewa ruzuku, basi Msajili wa Vyama vya Siasa ajiandae kusajili utitiri wa vyama.
“Msajili uwe tayari kusajili vyama laki moja, laki mbili. Hiyo changamoto nayo muiangalie,” alisema Marombwa. Vyama vingine vyenye usajili wa kudumu ni Tadea, Demokrasia Makini, Chausta, DP, Jahazi Asilia, AFP na CCK.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment