ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 30, 2014

Liberia yauona mwanga wa matumaini


Samantha Power na raisi Ellen Johson Sirleaf, hakuna kushikana mikono.

Shirika la afya duniani WHO limesema kwamba kuenea kwa ugonjwa wa Ebola nchini Liberia pengine kumepunguzwa kwa kiasi kikubwa,lakini ni mapema mno kusemba kwamba ugonjwa huo umedhibitiwa.

Kaimu mkurugenzi wa WHO,Bruce Ayward,aliwaambia waandishi habari kuwa idadi ya walioambukizwa uko wa Ebola iko palele haijaonhezeka,na maziko yamepungua.

Bwana Aylward amesema kwamba anaimani kuwa mapambano ya ugonjwa wa Ebola na virusi vyake sasa unaelekea kudhibitiwa.

Lakini ameeleza kuwa wataalamu wa Afya wanafuatilia kwa ukaribu mno kama kuna ongezeko lolote la idadi ya wagonjwa na vifo vipya, na kuonya kwamba ishara hiyo ndogo ya matumaini haina maana kwamba ugonjwa umedhibitiwa na haupo lah hasha. BBC

No comments: