Taarifa ya mrejesho wa kikao cha wanachama cha tarehe 12/22/2014
Wajumbe wamekubaliana kwa pamoja yafuatayo kama maazimio ya jumuiya.
Kutakua na vikao vinne kwa mwaka na kila mwanachama anatakiwa walau ahudhurie vikao viwili ili kuweza kuthibitisha uanachama wake katika jumuiya,,tofauti na hapo atakua amejiondoa mwenyewe.
Kujiunga katika jumuiya kama mwanachama ni hiari kwa wanachama wapya kama ilivyokua kwa wale wa mwanzo,
sifa kuu
ni uwe Mtanzania unaeishi MASSACHUSETTS USA na uweze kufuata sheria,mwongozo na taratibu zilizopitishwa na wanachama katika vikao vya jumuiya.
Malipo ya mchango wa jumuiya itaendelea kuwa kiwango kilekile $ 10 kwa mwezi na mwanachama asietoa kwa miezi mitatu mfululizo atakua amejitoa mwenyewe katika jumuiya na pesa aliyokwisha toa apo awali atorejeshewa.
Kiwango cha pesa za msiba toka katika jumuiya ni kiasi kilekile tulichokubaliana apo awali $ 3000 msiba ukiwa USA na $ 500 msiba ukiwa Africa. Makubaliano ni kwamba pesa hii itatoka katika Account ya jumuiya na kama kutakua na taarifa nyingine wanachama watataarifiwa
Wahusika katika kufiwa ni Mke,Mume,Mtoto wa kuzaa,Wazazi wawili na ndugu wa kuzaliwa damu moja.
N;B Kwa mawasiliano zaidi,
1.Idrisa Yusuph (Mwenyekiti wa muda 617-504-9804)
2.Halima Chunda (Makamu mwenyekiti wa muda 617-953-5375)
3.Shaban Sasillo (Mratibu wa jumuiya 571-224-5092)

No comments:
Post a Comment