Serikali imeshauriwa jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake ambao kwa sasa unalalamikiwa kwa sehemu kubwa na wananchi kwa kukiuka haki za binadamu.
Akizungumza jana mjini Dodoma katika kuhitimisha hoja kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa wa chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama wake,Mbatia alisema kuwa kitendo hicho kilikiuka haki za binadamu ikiwemo wanawake kudhalilishwa kijinsia.
Mh. Mbatia emeongeza kuwa ili chaguzi zijazo ziwe za amani na utulivu ameishauri serikali kubadilisha sera za vyama vya siasa na utawala pamoja na mfumo wa jeshi la polisi kuendeleza amani na utulivu ambavyo kwa sasa vinaonekana kuanza kutoweka.
5 comments:
Nilitoa mawazo wakati wa mchakato wa katiba katika ngazi mbalimbali, tunahitaji chombo mahususi cha kuichunguza polisi. Polisi hawawezi kuji - police - wenyewe. Yanapotokea matukio kama haya au hata ukiukwaji wa haki za washtakiwa, mafaili kupotea, kungekuwa na Police oversight body - ambayo inatengenezwa na wataalamu wa mambo mbalimbali ambao wangekuwa wanafuatilia na kuchunguza polisi. Tukiwaachia wao wenyewe, au commission za kuundwa ad hoc, haya mateso hayataisha. Hili ni muhimu kuliko mambo mengi tunayoyavalia njuga. Our police officers are above the law. What do you do? Call the police?
Uwezo WA police wenyewe kielimu Ni mdogo tuache kuajiri darasa la saba uwezo wao wakuchanganua sheria nimdogo ndioo maana wanachojua waoo nindioo mzee na kupiga..fools forever
Kwa lugha yako hii,naungana na Mh. Pinda,na wewe ni wa kupigwa tuu
msiwadharau watu wa darasa la saba nyinyi mkajifanya wasomi sana kumbe mafisadi watupu.
wewe huko ulipo hapo kazini kwako kama umeajiriwa una haki ya kumpiga mkuu wako thubutu. hata kama uko majuu thubutu na tena kazi zenu za vibaru ukichelewa mara mbili tatu kazi huna kaajiriwa mwinginewe na haa kaa una kazi nzuri huna ubavu wa kumpiga amri ya bosi watu na tena mtu mweusi mwenzangu ndo kabisa afadhali ungekuwa mzungu ungejaribu kubishana bishana mdogo mdogo na bosi but mweusi wenzangu ndo kabisa huna kauli.
so stop the bull mawe ya fisi kuwakandia mapolisi wamefuaa amri ya mkuu wao full stop wako kibaruani wanatafuta riski ili wawalishe familia zao full stop.
msijidai ujuajiji sana na usomi mbuzi,kama kusoma amesoma wa darasa la saba na kuhangaika na maisha si nyinyi mafisadi mitandaoni kuwananga wanafuata amri za mkuu wao.
Mdau hapo juu �� you're wrong, police wanachofanya ni kutiii amri na si vingine. Watu wa kulaumu ni politicians ambao ndo wako nyuma ya hii circus.
Post a Comment