ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 30, 2015

"MISHUMAA YA KALE" leo kama kawa.......USIKOSE

Photo Credits: Ye Olde Vivyl Shoppe
Baada ya pilika za wiki nzima, na mchamchaka wa maisha, sasa unakuja wakati wa kuburudika na muziki halisi wa zamani.
Katika kipindi hiki, utaweza "kuruka majoka" na "kula mangoma" kwa kusikiliza nyimbo ziliotamba miaka ya zamani, kupata historia ya wasanii na vikundi mbalimbali na pia kusikiliza mazungumzo na maDj na wasanii mbalimbali wa zamani.
Ungana na MixMaster Dj Luke Joe kwenye "one and two" na Mubelwa Bandio nyuma ya kipaza sauti kwenye kipindi kipya cha MISHUMAA YA KALE kitakachokujia kila Ijumaa kuanzia saa 11 kamili jioni mpaka saa 1 kamili usiku kwa majira ya Marekani ya Mashariki (5:00pm - 7:00pm EST)
Ungana nasi kupitia www.vijimamboradio.com ama  ama www.kwanzaproduction.com


3 comments:

Anonymous said...

Tunasubiri saa 11 jioni ifike, asante sana Bandio/DJ Luke

Anonymous said...

Jamani mnaweza kurudisha tena jumamosi? pia ijumaa itakuwa vyema kama mtarusha late kidogo instead of 5-7 pm naomba muanze angalau 7-9pm ili wachache tunaorudi kutoka kazini late nasi tuburudike! Mnaonaje dj Luke na Mubelwa?



Anonymous said...

Mi ndo kwanza nimetoka kazini. Naomba recorded version niburudike. Live siwezi kuwahi.