Na Mwandishi Maalum, New York
Katika kuhakikisha kwamba taarifa kuhusu vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini Tanzania zinawafikia watalii wengi na kwa urahisi nchini Marekani na kwingineko , jana ( alhamis) palifanyika onyesho la App inayotoa huduma hiyo kupitia Ipad, Iphone na Smart Phones.
App hiyo ijulikanayo kama “ Official Destination Tanzania, Zanzibar, Serengeti, Ngorongoro and Kilimajaro”, imeandaliwa Bi. Benita Cassar Tirreggian akisaidiwa na wataalam kutoka kampuni ya Apple kupitia mpango wao ujulikanao kama one to one.
Onyesho la App hiyo ambalo lilikuwa kivutio kwa wageni walioalikwa akiwamo Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, limefanyika katika duka linalouza bidhaa za Apple ambalo lipo katika Kituo Kikuu cha Treni ( Grand Central) jijini New York.
Baadhi ya washiriki kutoka TANAPA ambao wapo hapa New York kushiriki onyesho jingine la masuala ya kitalii maarufu kama New York Times Travel Show nao walihudhulia onyesho la App hiyo.
Akielezea ni kwa nini aliamua kutengeneza App hiyo, Bi. Benita aliwaeleza wageni waalikwa kwamba mapenzi yake mkubwa kwa Tanzania ndio hasa kulikochangia yeye kuamua kuitengeneza App hiyo ili uzuri wa nchi ya Tanzania, watu wake na maliasili zake ushuhudiwe na kuwavutia watu wengi zaidi.
Akaongeza kuwa pamoja na utaalam na usaidizi kutoka Kampuni ya Apple, Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wa sekta ya utalii, walimpatia ushirikiano mkubwa katika utengenezaji wa App hiyo ambayo anasema imeridhiwa na Serikali.
Balozi Tuvako Manongi alimshukuru Bi. Benita kwa uamuzi wake huo na pia akawashuru wageni mbalimbali waliohudhuria onyesho hilo huku akiwatia shime ya kwenda Tanzania kujionea na kufurahia utajiri mkubwa wa maliasili kwa maana ya mbunga za wanyama, bahari yenye kila aina ya vivutio na mengine mengi ambayo Tanzania imebarikiwa kuwa nao.
|
App inayoonyesha vivutio mbalimbali vya kitalii nchini Tanzania, App hiyo ambayo imeandaliwa na Bi. Benita Cassar Torreggiani kwa kusaidiwa na wataalam kutoka Apple inaweza kupatikana kupitia mitandao ya Ipad, Iphone na Smart Phone.
Mfanyakazi wa Apple Store Grand Centra jijini New York ambako onyesho hilo lilifanyika akimtambulisha Bi. Benita.
|
Balozi Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza na Bi . Benita ambapo alimshukuru kwa uamuzi wake huo wa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia App hiyo.
Hapa pia Balozi Manongi akiendelea na diplomasia ya Utalii akiwatia shime wageni waliohudhuri onyesho hilo kwamba wasiishie kuangali App bali wafike Tanzania washuhudie wenyewe.
Balozi Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza na Bi . Benita ambapo alimshukuru kwa uamuzi wake huo wa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia App hiyo.
Balozi Manongi akuzungumza na wageni waliofika kwenye onyesho ambapo pia alijibu baadhi ya maswali yao
Wageni wengine waalikwa
Balozi Manongi akibadilishana mawazo na wamiliki wa Kampuni ya Coastal Air Travel ambao wapo hapa New York kushiriki onyesho la New York Times Travel Show
Wawakilishi Kutoka TANAPA Dk. Ezekiel Dembe na Bw. Ibrahim Mussa ambao ni sehemu ya ujumbe wa Tanzania kwenye Onyesho jingine la masuala ya Utalii maarufu kama New York Times Travel Show nao walijumuika na wageni wengine kuangalia onyesho la App destination Tanzania.
Sehemu ya wagine wakifuatilia maelezo ya App hiyo kupitia screen zilizokuwa zilizowekwa ukutani katika eneo palipofanyika onyesho hilo
No comments:
Post a Comment