ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 25, 2015

BOKO HARAM 207 WAUAWA CHAD

Wanajeshi nchini Chad.

JESHI la Chad limetangaza kuwa, wanamgambo mia mbili na saba wa kundi la Boko Haram wameuawa katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.

Wanajeshi wa Chadi wakiendelea na ulizi katika eneo la Garambu lililoko katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.

Gazeti la Ufaransa la Le Figaro linaripoti kwamba, wanajeshi wa Chad wamewauwa wanamgambo mia mbili na saba baada ya kuzuka mapigano kati yao katika eneo la Garambu lililoko katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon.
Wanamgambo wa kundi la Boko Haram.

Mwanajeshi mmoja wa Chad ameuawa pia katika mapigano hayo huku wengine tisa wakijeruhiwa. Jeshi la Chad limetangaza pia kwamba, limefanikiwa kuchukua silaha na magari mawili ya Boko Haram yaliyoachwa na wapiganaji hao waliokimbia baada ya kuzidiwa nguvu.

Hivi karibuni nchi jirani na Nigeria ziliunda kikosi maalumu cha kupambana na wanamgambo wa Boko Haram baada ya kushadidi mashambulio ya wanamgambo hao na kuhatarisha usalama wa raia

No comments: