Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EY,Mark Otty akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokutana nao Februari 24,2015 kwenye ofisi za kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.
Meneja Mkazi wa Kampuni ya EY, Bw. Joseph Sheffu (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati walipokutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EY, Bw. Mark Otty (kulia) kuzungumzia ujio wake hapa nchini. Picha na Othman Michuzi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EY, Bw. Mark Otty, amesema Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo zinahitaji watu kuwekeza, hasa katika sekta ya miundombinu, kilimo, huduma za Kifedha ,mawasiliano,madini pamoja na gesi asilia .
Otty ameyasema hayo leo wakati wa alipokutana na waandishi wa habari kwenye ofisi ya kampuni hiyo hapa nchini,yenye makao yake makuu nchini Uingereza,amesema kutokana na rasilimali zilizopo zitavuta uwekezaji na uchumi wa nchi unaweza kukua.
Mkurugenzi huyo amesema kazi kubwa ya kampuni hiyo ni ushauri wa uchumi ,biashara pamoja na ukaguzi kwa sekta za serikali na sekata binafsi.
Amesema katika ziara yake nchini ni pamoja na kukutana na Rais Jakaya Kikwete na kujadili masuala mbalimbali likiwemo la ujio wake nchini na jinsi kampuni yake na serikali wanavyoshirikiana katika shughuli mbalimbali za biashara.
Kwa upande wa Meneja Mkazi wa Kampuni ya EY, Bw. Joseph Sheffu amesema kuna maeneo mengi wameayatafiti na kuona kuna fursa ya uwekezaji kutokana na taratibu bora zilizopo nchini katika sekta ya uwekezaji.
Bw. Sheffu amesema kampuni hiyo ina wahasibu,wataalam wa kodi pamoja na wakaguzi ambao wameweza kupata ujunzi katika mataifa mbalimbali hivyo huduma inayotolewa na taasisi hiyo imekuwa ni bora.
No comments:
Post a Comment