ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 26, 2015

DALILI 5 KWAMBA MPENZI WAKO ANA WA KUMCHUNA!

Mapenzi ya sasa yamejaa usanii wa hali ya juu. Wapo wanaume ambao wana wapenzi wao lakini ukiwafuatilia utagundua wana ‘mashuga mami’ ambao wanawapa jeuri ya fedha.

Ukiachilia mbali hao wanaume, wapo mabinti ambao licha ya kuwa na wapenzi wao wanaowapenda, pembeni wana wanaume wa kuwachuna.Utajuaje kama wa kwako naye ana mtu anayemchuna? Dalili hizi 5 ni kati ya nyingi zinazoweza kukupa mwanga.

Ana simu zaidi ya moja
Najua wapo wasichana ambao kutokana na majukumu yao, wanalazimika kuwa na simu mbili au zaidi. Wengine wanakuwa na simu moja lakini yenye line mbili au tatu.Hata hivyo, ukiona mpenzi wako ana simu mbili lakini wewe kakupa namba moja, ujue anazo namba kwa ajili ya kuwasiliana na wanaume wengine.

Inatakiwa kuwa hivi, kama una mpenzi wako ana line tatu kwa sababu maalum, lazima wewe kama mpenzi wake ujue. Endapo atafanya siri, kisha ukajua basi ujue yupo mwanaume mwingine anayewasiliana naye kwa siri.

Matanuzi zaidi ya kipato
Unaweza kuwa na mpenzi ambaye huenda unajua ana kipato gani na wewe huwa humpi pesa nyingi. Pia yawezekana unajua familia yake haina fedha kivile. Sasa katika mazingira hayo ukiona ana matanuzi ya kutisha itakuwiaje ngumu kuhisi kuna mtu mwingine wa pembeni anampa jeuri?

Kwa mfano unamuona mpenzi wako ana simu kali zaidi ya moja, kila siku anabadili mavazi ya gharama na huenda siku mojamoja unamuona na usafiri, bado utakubali matumizi yake hayo ni halali? Akili kumkichwa.

Ukimhitaji anatoa udhuru
Mpenzi wako anayekupenda kwa dhati ni yule ambaye ukimhitaji, mtakutana. Endapo utakuwa na mpenzi ambaye anakuche-ngachenga, huenda wakati wewe unamhitaji tayari ana miadi ya kukutana na mtu ambaye anampa jeuri ya pesa.

Ukweli ni kwamba, wasichana wengi wa sasa wanathamini sana wanaume wanaowapa pesa, matokeo yake sasa unaweza kujikuta wewe unayempenda kwa dhati unanyanyaswa, yule ambaye ni mtoaji wa pesa, asiyeona hatari kumhudumia msichana hata kama ana mtu wake, ndiye ‘anayeinjoi’.

Mawasiliano tata ya simu
Mtu aliye kwenye uhusiano kutopokea simu ya mpenzi wake au kutokuwa hewani kwa muda mrefu huwafanya wengi wahisi wanasalitiwa.

Hata hivyo, usijiaminishe sana kwenye hilo kwani wapo ambao wana uwezo wa kupokea simu za wapenzi wao hata kama wapo na michepuko.Kwa mfano unaweza kumpigia simu mkeo, akapokea na kuongea na wewe kwa mahaba kabisa kiasi kwamba huwezi kuhisi yuko gesti na mwanaume mwingine.

Lakini kumbe mwanaume aliyenaye anajua ni mwizi na wala hawezi kumkataza kupokea simu.
Licha ya ukweli huo, bado ukiona mpenzi wako mara nyingi unampigia simu hapokei bila sababu au anazima simu bila kukutaarifu, hiyo ni dalili kwamba huenda muda huo yuko na mchepuko.

Mashosti zake wachunaji
Ukiona mpenzi wako ‘anaiva’ sana na mabinti wa mjini ambao hawana kazi za maana lakini mambo yao safi, ujue na wako hawezi kukwepa mitego ya wanaume wakware.

Hata kama anakupenda kwa dhati na haoneshi kuwa na tamaa ya pesa, unaweza kushangaa wenzake wanamshawishi na kujikuta anaingia mkenge, hasa pale ambapo wewe unaonekana kuwa mgumu wa kumhudumia au unatamani kumpa kila anachokitaka lakini huna uwezo. Hizo ni dalili chache ambazo ukiona mpenzi wako anazo, fuatilia huenda ukagundua hauko peke yako.

GPL

No comments: