Akimsomea mashitaka, Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alisema Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake aitwaye Bahati Kabanda 'Masika'.
Alisema kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka jana ambapo meneja huyo alikwenda kwenye baa hiyo kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo.
Hakimu Msuya alisema kuwa Cheka alikataa kumlipa na kumshushia kipigo kilichosababisha kulazwa hospitalini.
Baada ya hukumu hiyo huku Cheka akipandishwa kwenye difenda tayari kupelekwa gerezani akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote, mashabiki wake walimvaa meneja huyo wakitaka kumshushia kipigo hivyo kuibua taharuki mahakamani hapo.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakisema wapo tayari kujichanga ili kukata rufaa wakiamini kuwa bondia huyo ameonewa. GPL
Mbali na hukumu hiyo mahakamani hapo, kulikuwa na kesi nyingine mbili zilizokusanya umati, moja ikiwa ni ya Sheikh Ponda juu ya uchochezi na ile ya mtoto wa boksi inayowakabili baba na mama Nasra.
1 comment:
Watanzania tuelimike. Sheria siyo ya wakuwalinda watu maarufu tu. Muda umefika wanyonge nao kupata haki yao. Kazi nzuri sana hakimu. Ubondia ni mchezo siyo ubabe kwa mtu anaye kudai. Natumai watu wengine kama cheka watajifunza.
Post a Comment