ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 3, 2015

Juan Quadrado atua Chelsea, Fletcher wa Man U atimkia West Brom, Andre Schurrle ameuzwa Wolfsburg

image
imageChelsea wamemsajili winga Juan Cuadrado kutoka Fiorentina, katika biashara kubwa zaidi iliyofanyika siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo.

Jose Mourinho alikuwa akidai kwamba hawangesajili mchezaji yeyote wakati huu, lakini wametoa pauni milioni 23.3 kumnasa mchezaji huyo, na kufanya jumla ya fedha zilizotumiwa na klabu za ligi kuu kwenye usajili huu kufikia pauni milioni 130.

Matumizi hayo ni sawa na ya kipindi kama hiki msimu uliopita, lakini ni madogo zaidi ya Januari 2011 yaliyokuwa pauni milioni 225. Mchezaji mkongwe wa Manchester United, Darren Fletcher amehamia West Bromwich Albion, kutokana na kukosa uhakika wa muda wa kucheza.

Crystal Palace wamesajili jumla ya wachezaji wanne, wengi kuliko klabu nyingine yoyote, ikiwa ni pamoja na kumnunua kinda wa Man United, Wilfried Zaha.

Hull wamemsajili mshambuliaji wa Lokomotiv Moscow, Dame N’Doye, Chelsea wamemuuza moja kwa moja Ryan Bertrand kwa Southampton wakati Tottenham Hotspur wamemtoa kwa mkopo Aaron Lennon kwa Everton.

Robert Huth ameondoka Stoke kujiunga na Leicester kwa mkopo, ambapo klabu hiyo inayopambana kushuka daraja pia imemsajili kiungo wa Bolton, Lee Chung-yong na matineja Andreas Breimyr na Keshi Anderson.

Spurs wametangaza kumchukua kiungo wa MK Dons, Dele Alli kwa ada inayodhaniwa kuwa kwenye pauni milioni tano.

Usajili zaidi uliofanyika wakati huu ni kwa Chelsea kumuuza Andre Schurrle kwa Wolfsburg kwa pauni milioni 22, kumtoa kwa mkopo Mohamed Salah kwa Fiorentina katika dili lililomleta Cuadrado Stamford Bridge. Kwa msingi huu, Chelsea wametengeneza faida Januari hii.

Kiungo Filip Djuricic amesajiliwa Southampton kwa mkopo kutoka Benfica. Manchester City ndio wameongoza kwa kununua mchezaji ghali zaidi Januari hii, kwa kumsajili mshambuliaji Wilfried Bony kutoka Swansea kwa pauni milioni 28.

Arsenal nao walifanya biashara yao kwa kumsajili beki wa kati wa Villarreal, Gabriel Paulista kwa pauni milioni 11. Leicester walivunja rekodi yao ya kutumia fedha nyingi kwenye usajili kwa kumchukua mshambuliaji wa Croatia, Andrej Kramaric kwa pauni milioni tisa.

Tanzania Sports

No comments: