ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 4, 2015

JACQUELINE NTUYABALIWE AACHA HISTORIA

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Abraham Mengi akiongea maneno ya kuapa na kumvisha pete ya ndoa Miss Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe 'K-Lyn' wakati wakifunga ndoa.
Mengi akimkumbatia K-Lynn kama ishara ya upendo.
Maharusi wakipiga picha ya pamoja. Wa pili kushoto ni Nancy Sumari (Miss Tanzania na Miss World Africa 2005) na mumewe Luca ambaye pia ni mmiliki wa mtandao wa Bongo5.
Maharusi na wapampe wao wakitembea ufukweni sambamba na watoto wao mapacha.
wakirusha maua na kufurahia.

MISS Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe ameacha historia ya aina yake nchini, baada ya kufunga ndoa na Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Abraham Mengi, tukio lililofanyika nchini Mauritius mwishoni mwa mwezi uliopita.

Jack, ambaye pia anafahamika kwa jina lake la kisanii kama K- Lynn, anaacha historia hiyo nchini Tanzania kwani licha ya kufunga ndoa hiyo akiwa tayari na watoto wawili mapacha aliozaa na mumewe, pia ndiye mshindi wa kwanza wa shindano hilo kubwa, kuolewa na bilionea baada ya kuwa katika uhusiano kwa miaka kadhaa pasipokuwa na kashfa na miezi minne baada ya kuvalishwa rasmi pete ya uchumba.

K-Lynn ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, anaweka pia historia hiyo kwa kuolewa na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa na wenye kuheshimika katika Afrika Mashariki, ambaye licha ya kumiliki vyombo vikubwa vya habari vikiwemo redio, magazeti na televisheni, pia ni mmiliki wa viwanda, migodi ya madini na biashara nyinginezo kubwa. IPP inamiliki vituo vya Radio One, Capital Radio, East Africa Radio, ITV, Eatv, Capital TV na magazeti la Nipashe, The Guardian na mengine kadhaa.

Harusi yao inayotajwa kuwa ni moja kati ya ndoa za kifahari nchini Tanzania, ilihudhuriwa na idadi ndogo ya watu wapatao 50, ambao ni ndugu wa karibu wa familia hizo mbili, pamoja na marafiki muhimu wa pande zote mbili.

Mengi, anayetajwa kuwa tajiri wa tatu nchini, miezi minne iliyopita, alimvalisha pete ya mchumba msanii huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa wa kufanya muziki, wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na watu wachache.

Baadhi ya washindi wengine wa shindano la Miss Tanzania walioolewa ni pamoja na Hoyce Temu (1999), Miriam Magese (2001) Faraja Kota (2004), Nancy Sumari (2005) na Sarah Israel (2011).



STORI: OJUKU ABRAHAM/GPL. PICHA: BONGO5

9 comments:

Anonymous said...

Kuzaa watoto bila ya kuwepo ndoa sio scandal?Jamani tumuogopeni Mungu

Anonymous said...

Ndo hapo ujiulize, watu wanakaa vimada wanazaa watoo bila ndoa halafu wanakuja jitakatisha na misifa hisio na nyuma wala mbele. Hapa inhekuwa mtoto wa Tandale na Zari yangesemwa mengi, na kuitwa majina yote machafu!! $$- wabongo tunasujudu sana pesa

Anonymous said...

please be sensible. kuzaa kabla ya ndoa yaongenei hayo misikitini ama makanisani. chaguo la mtu ni uamuzi wake. wish them the best or keep ur silence.

Anonymous said...

Kweli pesa ni sabuni ya roho,kweli huyu binti angetokewa na mzee kingwedu angekubali?

Anonymous said...

Kioo cha jamii Mzee Mengi anafundisha watoto wasijibidishe na maisha kwani hali ikiwa mbaya unaolewa na babu zao! Kisaikolojia Mengi kafilisika! hajitambui ! kujifanya wamo wakati science insema uko hoi, unahitaji mapumziko! aibu

Anonymous said...

Good point. Kuzaa bila ndoa kama ni kosa basi ni kati ya wanaadamu na muumba wao. Siku ya haki kila mwanadamu atasomewa mema yake na mabaya yake. Siku hiyo itajulikana wapi walifanya mema na wapi walifanya mabaya. Wewe ongelea yanayokuhusu. Tuanze nawe -Unauhakika ulipozaliwa wazazi wako walikuwa kwenye ndoa? au ni ya kimila? je wewe sio mtoto wa nyumba ndogo? na wanao je wote wataolewa na kuoa? Na nduguzo? Mind your own business people

mchumi said...

Pesa inathungumusa

mchumi said...

Pesa inaongea

Anonymous said...


Habari haijaandikwa vizuri, lakini ni bora kuzaa nje ya ndoa kuliko kufanya abortion. Pia hata kama walifanya kosa, kwani wao hawastahili kusamehewa?