ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 17, 2015

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA TUME YA UKIMWI AZIKWA LEO ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia akijumuika na Viongozi na Waislamu mbali mbali katika kumswalia aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri katika Msikiti wa Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja kabla ya mazishi yake leo,[Picha na Ikulu.]
  Baadhi ya wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakilibeba jeneza la aliyekuwa katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sherif na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (katikati) wakiwa na Viongozi wengine na Wananchi katika mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo  kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(katikati)akitia udongo kufukia kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar Marehemu Dkt.Omar Makame Shauri aliyezikwa leo  kijijini kwao Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Unguja.

1 comment:

Unknown said...

Inna Lillahi Waina Ilahi Rajiun. May Allah forgive your sins and grant you Jannatu Firdaus. The pictures give us comfort those of us who could no be there. You will be forever in our hearts. May you rest in peace. Your Niece