Mikutano ya majira ya Kipupwe imeanza rasmi tarehe 14/4/2015 na kuhudhuriwa na nchi mbalimbali wanachama zaidi ya 188. Mikutano hii huudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi kutoka serikalini, waandishi wa habari, Mashirika na Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi pamoja na kamati za kifedha.Taasisi hizo kwa pamoja zitajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Tanzania ni nchi wanachama katika Mikutano hiyo.Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB), aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi na manyunyu ya hapa na pale.
Imetolewa na:
Msemaji wa Wizata ya Fedha
Ingiahedi C. Mduma
14/4/2015
Washington DC.
No comments:
Post a Comment