ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 15, 2015

WACHOTA MAJI "TAKA" KWA MATUMIZI YA NYUMBANI

Mama huyu mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, akichota maji yanayovuja kutoka kwenye bomba la la maji ambayo hata hivyo yamechanganyika na maji taka yanayotiririka kama yanavyoonekana kutoka kupande wa juu kushoto wa picha hii iliyopigwa Jumanne Aprili 15, 2015. Uchunguzi wa K-VIS blog umebaini kuwa maeneo ya Mabibo na Kigogo, yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji ambapo sasa wakazi wake hususan akina mama na watoto wamekuwa wakiyatafuta hata yanapoonekana yakiwa kwenye mazingira ya uchafu, ambapo wengine wameonekana wakichota kwenye mitaro ya kupitishia maji machafu
Hapa ni barabarani eneo la Kigogo Randa Bar
Barabarani Randa Bar Kigogo
Mtaroni eneo la Mabibo
K-VIS Blog

5 comments:

Anonymous said...

Bongo tambarareeeeeeeeeee

Anonymous said...

Ndio legacy ya miaka kumi ya Kikwete

Anonymous said...

Hivi kweli, we can justify multiple $30 million+ purchases of the buildings za balozi around the world while this is kind of life 98% of the people are living? What a load of crap is this? No wonder they are using a lot of energy to justify the purchase of NY Tanzania House. It doesn't make sense! Kwa wale watakokuja kwa hoja ya it's better to buy than to rent, I'm going to tell them that they are wrong. Even if you were paying a $35,000 per month for leasng, it would take you 867+ Months to come out even (given the rate of inflation and maintenance). It is simply a wrong way to approach the problem of it is a problem. Use the funds to fix these social issues at home and believe me the impact is HUGE!
Mdau,
Missouri

Anonymous said...

Kweli ndo maendeleo hayo mnawashauri watu warudi bongo?ebu rekebesheni mambo kwa kila mtu msiwe wabinafsi mnajali familia zenu?hali hiyo ni mbaya.

Anonymous said...

Asante kwa kutujuza. Napenda kuipongeza K-VIS Blog kwa kutoa picha hizi. Blogu zingesaidia sana kama zingetoa kipaumbele habari zenye faida kwa jamii badala ya makalio ya wanawake kwenye intagram