ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 7, 2015

MTOKO WA PASAKA WA GWT ULIVYOFANA SIKUKUU YA PASAKA

Waimbaji wa Glorious Worship Team (GWT) wakiwa stejini wakati wa kumsifu Mungu na kumwabudu.
Glorious Worship Team wakizidi kumwabudu Mungu katika Ukumbi wa Victoria Petrol Station.
Mpiga gitaa la sauti nzito (base) wa GWT, Emmanuel Materu akicharaza gitaa hilo. Pembeni yake ni waimbaji wenzake.
David Silomba (kulia) pamoja na Paul Clement wakiendelea kutoa burudani.

Kutoka kulia ni mwimbaji David Silomba akiimba sambamba na Editha Salum. Katikati ni Mpiga gitaa la sauti nzito (base), Emmanuel Materu.
Davina Lema (kulia) na Mary Igoti wakimwabudu Mungu wakati wa hafla ya Mtoko wa Pasaka.
Mwimbaji Editha Salum akizidi kumtukuza Mungu.
Dk. Mponzi pamoja na familia yake wakiwa na wadau wengine wa GWT wakati wakifuatilia matukio mbalimbali ukumbini hapo.
Ester Peter (kulia) akiimba pamoja na Salome Shemakulenge.
Mlezi wa GWT, Eric Shigongo akisalimiana na mmoja wa wadau wa GWT.
GWT wakiendelea kumsifu na kumwabudu Mungu kwa nyimbo.
KIKUNDI cha kumsifu na kumwabudu Mungu cha Glorious Worship Team (GWT) katika Sikukuu ya Pasaka kilitoa burudani ya nguvu kwenye hafla ya kumsifu na kumwabudu Mungu iliyokwenda kwa jina la 'Mtoko wa Pasaka' na kufanyika Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo, GWT walimsifu na kumwabudu Mungu kwa nyimbo ikiwa ni muendelezo wa programu yao ya Sunday Celebration ambayo hufanyika kila Jumapili kuanzia saa 9 alasiri baada ya ibada.
Akizungumza na mtandao huu, Mkurugenzi wa GWT, Emmanuel Mabisa amesema wiki hii katika Sunday Celebration Season 4 ndani ya Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Mjasiriamali na Mtunzi mahiri wa Vitabu, Eric Shigongo ataendelea kutoa somo lake la Siri za kutoka kuwa Mwajiriwa hadi kuwa Mwajiri.
Katika somo hilo, Shigongo atatoa bure vitabu vyake zaidi ya 200 alivyoahidi kuvitoa kwa watu waliowahi kufika ukumbini katika Sikukuu ya Pasaka.
Waimbaji mahiri wakiwemo; Upendo Nkone, Carvary Band, The Jordan Moses Zamangwa (Mosax), na Masanja Mkandamizaji watakuwepo kutoa burudani siku hiyo ya Aprili 12, mwaka huu.

1 comment:

Anonymous said...

Hili neno LA mtoko kama mngeangalia maana yake katika kamusi sidhani kama mngeliandika