Zari na Sempala wakipozi kimahaba.SEMPALA ACHUKIA UHUSIANO WA ZARI, DIAMOND
Kati ya watu wa mwanzo walioponda uhusiano wa Zari na Diamond ni Sempala ambaye alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo akisema kwamba hapendezwi kabisa na pea ya wawili hao.
Habari zilieleza kwamba Sempala ambaye anasifika kwa dili za mjini, anaonekana kutokuwa katika hali ya kawaida tangu alipopigwa chini na Zari mwaka jana hivyo kuchukuliwa kama anasema chochote kutokana na kuchanganyikiwa.
Juhudi za kumpata Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akitarajia kupata wa nne, aliyeko nchini Afrika Kusini ’Sauzi’ ili kusikia upande wake juu ya sakata hilo, ziligonga mwamba hivyo zinaendelea.
Diamond alipotafutwa na kunyetishiwa ishu hiyo alisema kuwa hana la kusema na hawezi kushindana na midomo ya watu.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.
Hasira ya kibuti? Ubuyu kutoka nyumba ya jirani, Kampala nchini Uganda unaeleza kuwa mwanaume Farouk Sempala aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
ameibuka na madai mazito kuwa mwanamama huyo alichoropoa mimba zake zaidi ya mbili.
TUJIUNGE UGANDA
Katika mahojiano maalum na Gazeti la Red Pepper la nchini humo hivi karibuni, Sempala alifunguka kuwa alishtushwa na habari kuwa mwanadada huyo alikutana na Diamond kwenye ndege na kuanza projekti ambayo matokeo yake ni mimba.
MIMBA ZAIDI YA 2
Jamaa huyo alidai kuwa, wakati akiwa kwenye mapenzi na Zari baada ya mwanamama huyo kutengana na mumewe, Ivan Semwanga, alitoa mimba zake zaidi ya mbili hivyo anaamini kuwa hata hiyo ya Diamond anaweza kuichoropoa.Sempala alisema kuwa katika kipindi cha mapenzi yao, walikuwa hawatumii kinga hivyo Zari alikuwa akinasa mimba lakini akawa anachoropoa.
“Tulifanya ngono laivu tena mara nyingi tu bila kinga.
“Katika kufanya hivyo nilimpa mimba siyo mara moja wala mbili lakini alikuwa akizichoropoa.
“Kamwe Zari hakunipenda. Alichotaka ni kumuonesha tu Ivan (aliyekuwa mume wa Zari) kwamba alikuwa amepata mwanaume mwenye misuli,” alianika siri zao Sempala katika gazeti hilo.
AMECHUKUA HATUA GANI?
Alipoulizwa juu ya hatua alizochukua au anazotarajia kuzichukua kwa Zari, Sempala alisema hakuna hatua atakayochukua lakini ameamua kusema juu ya uchoropoaji huo wa mimba akiwa na wasiwasi kuwa huenda hata hiyo ya Diamond ataichoropoa hivyo achukue tahadhari.
GUMZO
Habari kutoka kwa chanzo chetu chenye maskani yake Chuo Kikuu cha Kampala (Kiu) nchini Uganda kililitonya Amani kwamba, baada ya habari hiyo kuingia mitaani iligeuka gumzo kubwa huku wengi wakieleza kuwa huenda Sempala ameamua kumchafua Zari kwa sababu mwanamama huyo alimpiga kibuti cha kihistoria.
“Yaani gumzo hapa Kampala ni habari hiyo ambayo imetoka kwa ukubwa kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti.
“Unajua huyu Sempala bado kiroho kinamuuma. Kinachoonekana anatapatapa kwa sababu Zari alimpiga kibuti kibaya na cha ghafla kisha akanasa kwa Diamond,” kilisema chanzo hicho.
3 comments:
Diamond huna cha kutudanganaya!! huyo sio mke bali umepotea na nakuhakiki hutadumu naye kwa muda wa miaka miwili tunavyokujua kiwembe na kuchanga kwa wingi bora ungempata aliyetulia!! umechemka.. buuuhh..
So what? you own her Kizazi? Zari like any other woman can decide for her life. You were not good enough then. Zari has a right to have children like any other adult woman. This is soo annoying that some men think they can own women like property.
Well said mdau hapo juu. Just because I do with you it doesn't mean I want your offspring!! Siyo kila mwanaume wa kuzaa naye.
Zari is real woman she knows what she wants, and it seems she got it in Diamond's hands, so why not having a baby with him yo give what Diamond wants and make it a fare game!!
Wanaume wengine wanapotray wako nice in public eyes kumbe ni wakorofi sana, you never know what Zari experienced in her past relationships mpaka aamuwe kuwa na kijana wa Tandale. Obviously she was looking for a true love, I said true love not perfect love as that doesn't exist!!
Na wewe mdau wa kwanza embu funga mdomo wako, kama unajiamini embu comment kwa jina na sura yako hapa tukuone. Zari hajatulia? You have never been in her shoes so don't judge her! Ngedele wee!!
Post a Comment