ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 30, 2015

YANGA YA KIMATAIFA YAPANDA PIPA KUELEKEA TUNISIA




Viungo wa Yanga Andrey Coutinho (kushoto) na Nizar Khalfan nao walikuwa sehem ya wachezaji waliosafiri kuelekea Tunisi
Kocha mkuu wa timu hiyo Hans van der Pluijm amesema, hawana cha kupoteza kwenye mchezo huo hivyo wanahitaji kuibuka na ushindi ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.
“Hatuna cha kupoteza kwenye mchezo huo, tulitoka sare ya kufungana goli 1-1 tukiwa nyumbani hivyo tunahitaji kupata ushindi au sare ya magoli kuanzia mawili ili tuweze kusonga mbele. Tumejipanga vizuri kwa hili na wachezaji wote tunaokwenda nao wanatambua umuhimu wa mchezo huo”, amesema Pluijm.
“Etoile ni timu nzuri na inauzoefu mkubwa kwenye michuano ya Afrika na kila mtu aliona aina ya soka walilocheza hapa, tunawaheshimu na tumejipanga ili kukabiliana nao na kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo”, aliongeza Pluijm.
“Ni lazima tucheze soka la kushambulia na kupata magoli ya mapema lakini wakati huohuo tunatakiwa kuwa makini sana kuhakikisha haturuhusu kufungwa goli, nimezungumza na wachezaji na kila mtu anajua majukumu yake. Najua kwenye soka lolote linaweza kutokea na tukasonga mbele kwa hatua inayofuata”, alimaliza Pluijm.
Wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye foleni wakisubiri kukaguliwa hati zao za kusafiria kabla ya kuondoka
Kikosi cha timu ya Yanga kimeondoka usiku huu kuelekea Tunisia kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Etoile du Sahel utakaopigwa nchini humo siku ya Jumamosi.
Kikosi cha Yanga kimeondoka na msafara wa watu 50 wakiwemo wachezaji, viongozi, benchi la ufundi pamoja na wanachama na wapenzi wa timu hiyo. Msafara huo wa Yanga unaongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF Ayubu Nyezi, wameondoka kwa ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai hatimaye kutua Tunisia.
Credit:ShaffihDauda.com

No comments: