MKUTANO Mkuu wa Dharura wa Wanachama wa Klabu ya
Coastal Union unatarajiwa kufanyika kesho Mei 17 mwaka huu kwenye
ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Tanga.
Sababu za Mkutano huo kufanyika katika Ukumbi la
Polisi Mesi ni
kutokana na makao makuu ya klabu ya Coastal Union
kuendelea mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa na upigaji picha
wananchikwa ajili ya vitambulisho hivyo.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar
Assenga alisema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri na
unafanyika kufuatia vikao vya maridhiano ya Uhakikiwa wanachama wa Klabu ya
Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.
Ambapo alisema baada ya kumalizika vikao
hivyo,Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliiandikia barua Klabu ya Coastal
Union akiiagizklabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe
17 Meimwaka 2015.
Alisema kuwa matokeo ya maamuzi haya
yamepatikana baada ya kikao chausuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji yaTFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu
Mkurugenzi waSheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter
Mvella kilichofanyika April 13 mjini hapa.
Aidha alisema kuwa tayari shirikisho la soka nchini
(TFF) ilishatuma
orodha tatu za majina Wanachama stahiki,Wanachama
waliobainika kuwawanadosari na inabidi wathibitishwe na wanachama stahiki.
Orodha nyengine ni waombaji wapya wa wa
uanachama watakaohakikiwa nawanachama stahiki ambapo utaratibu huo ndio
ulioagizwa kutumika .Hata hivyo alisema kuwa orodha zote zimekwisha kubandikwa
kwenye ubao waMatangazo wa Klabu ya Coastal Union tayari kwa ajili ya mkutano
huo wa kesho.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Coastal Union.
No comments:
Post a Comment