ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 8, 2015

MWENYEKITI WA RED CROSS MKOA ARUSHA AKABIDHI MSAADA KWA WALEMAVU


Na Cynthia Mwilolezi, Arusha


CHAMA cha Msalaba Mwekundu (Red Cross), Mkoa wa Arusha, kimetoa msaada wa vyakula, viatu, Blanketi na nguo, kwa wazee nane na watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali 22, ikiwa ni maadhimisho ya chama hicho Duniani, ambapo kilele chake Mei 8 kila mwaka.

Akizungumza leo Jijini Arusha, wakati akikabidhi misaada hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba mwekundu Mkoa wa Arusha, Christopher Nzera, amesema kuwa misaada hiyo ni moja ya shughuli zao wanazofanya za kusaidia jamii na watu wasio na uwezo .

Nzera ametaja vitu walivyotoa ni pamoja na mchele, nguo za kike na kiume, sabuni, viatu na fedha kiasi, ili waweze kumudu maisha yao kwa siku chache.

Aidha amesema katika maadhimisho hayo wameamua kujitolewa uchangiaji
wa damu salama toka kwa wanachama wa chama hicho na kisha itapelekwa
hospitali ya Mkoa Mount Meru Arusha, ili iwasaidie wahitaji wanapopata ajali na majanga mengine.

Amewaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kupenda kujitolea damu kwa ajili
ya kuokoa maisha yaw engine, badala ya kusubiri wakati wwa majanga pekee.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Mkoani Arusha, Phillipo Nery, ameshukuru msaada huo umefika wakati muafaka, wakati wanaelekea kipindi cha baridi Mkoa wa Arusha.

Amesema pamoja na msaada waliopata bado walemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ukosefu wa matibabu, licha ya serikali
kuwaahidi kuwapatia bure, lakini kama wazee wameishia kupata vipimo na
kufunguliwa mafaili, ila dawa wanatakiwa kununua wenyewe jambo ambalo
gumu kwao.

No comments: