ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 8, 2015

SUNGUSUNGU WA MANISPAA YA SHINYANGA WAPEWA PIKIPIKI KUKABILIANA NA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE



Katika kukabiliana na vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino),leo jeshi la jadi sungusungu katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga limekabidhiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja, laki 6 na elfu 50 kwa ajili ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ambapo alisema ingawa katika manispaa hiyo hapajaripotiwa tukio la mauaji ya albino,pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha zaidi ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

Zoezi la makabidhiano limefanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo.


Pikipiki hiyo imetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kupitia kwa mfanyabiashara Ndegesela na kukabidhiwa kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga, James Deshi.Pichani katikati ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro ambaye naye alikabidhi ufunguo huo kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.

Akikabidhi pikipiki hiyo meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alisema pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

Matiro alisema wataendelea kutoa msaada wa pikipiki  kwa jeshi la sungusungu katika kata 17 za manispaa hiyo na mwezi Juni mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele atatoa pikipiki 2 kwa jeshi hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na  viongozi wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga
Viongozi wa Jeshi la Sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiondoka na pikipiki waliyokabidhiwa,anayeendesha ni katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga.

No comments: