chanjo ya kuzuia mimba
Wanawake wa Kenya hawataki kuwa na wajukuu mapema.hawataki kuwa mabibi ilhali watoto wao wa kike wakiwa chini ya umri wa miaka 18.
‘’Hofu yao , hasa wamama waishio mjini ni kuwa hivi sasa wanawapa watoto wao wa kike wenye miaka 12 sindano za uzazi wa mpango wakihofu kuwa mabiti zao watapata ujauzito na kukatiza masomo.
Hivi sasa wanajaribu kila njia za uzazi wa mpango ili angalau mabinti wamalize elimu ya Sekondari’’.Wycliffe Onkendi, Ofisa kutoka Wizara ya Afya ambaye amefanya kazi eneo la Rift Valley ameeleza.
Kulingana ana gazeti la the Standard matumizi ya njia za uzazi wa mpango kunamaanisha kuwa wanawake hawa wamekubali kuwa mabinti zao wanajihusisha na ngono zisizo salama wangali na umri mdogo.hofu yao hasa imejikita katika madhara ya kupata mimba zisizopangwa kabla ya kumaliza masomo.
Mary Agak, ni Mama na mfanyabiashara mjini Kericho anasema’’ binti yangu yuko kidato cha tatu huwa tunaongelea maswala haya mara chache na wanawake wengine kwenye chama sioni kama ni makosa.kabla ya kuingia kidato cha tatu nilimpeleka kuchomwa sindano ambayo ilikaa kwa miezi mitatu mpaka mine ni vijana wadogo damu inachemka huwezi jua watafanya nini’’.Chanjo ya kuzuia mimba
Mama mwenye watoto watatu anaongeza ‘’bora nizuie balaa hili kuliko kumshuhudia asimalize shule’’.
Ofisa mmoja katika Zahanati moja mjini Eldoret Paul Anyango anasema ‘’mabinti walio Sekondari hufika kwenye kituo hicho cha afya wenyewe kwa ajili ya kupata vipandikizi au sindano wanapokwenda shuleni’’
Hali hii inafanya watu kujiuliza mabinti hawa hufanya nini zaidi ya masomo wanapokuwa shuleni.
No comments:
Post a Comment