Mkoa wa Kagera
umebarikiwa kuwa na uwakilishi mzuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya
nchi, mfano mzuri ni Mwanamuziki wa kike
Abela ambaye ni mzaliwa wa Bukoba Mkoani Kagera anayepeperusha vyema bendera ya
Tanzania kimziki huko Amerika anakoishi na kufanya kazi zake za muziki.
Abela Kibira alizaliwa
Septemba 22 mwaka 1989 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya Mtanzania Josiah
Kibira mzaliwa wa Bukoba Kagera, Tanzania na Mmarekani, Mrs Josiah Kibira.
Mchanganyiko huo wa tamaduni mbili kwa binti huyo ambaye ana kipaji cha utunzi na uimbaji, umemfanya kujimarisha na kujijengea jina katika muziki kutokana na aina ya muziki na manjonjo anayoyafanya katika mzuiki wake kupendwa.
Abela ni mzaliwa wa
Bukoba, Tanzania lakini kwa sasa anaishi Minneapolis, Marekani. Binti huyu
anasauti nzuri, ya kipekee na ya kuvutia jambo ambalo nyimbo zake nyingi
zimekuwa zikipendwa sana
Onyesho lake la kwanza
Binti huyu alilifanya kanisani na ndipo kipaji chache kilipojifunua machoni mwa
watu wengi na hivyo kuendelea kuimba katika matamasha mbalimbali shuleni na
matamasha maalumu.
Abela amekulia katika
mji wa Wayzata, Minnesota na alipendwa kutokana na kuwa na uwezo wa ajabu
katika kuimba kwaya na matamasha ya pamoja wakati akiwa katika masomo yake ya sekondari
na chuo.
Mwaka 2003 baba yake
mzazi Mr. Josiah Kibira alimshirikisha katika filamu yake aliyoiita Bongoland,
ambapo Abela alitunga wimbo wa kusindikiza filamu hiyo (soundtrack) jambo
lililomuongezea uwezo na umaarufu kwa mashabiki Amerika, Afrika na maeneo mengi
ulimwenguni.
Abela ambaye bado
binti kigoli anayejitambua amekuwa akiiimba na kujifua utumiaji wa sauti takriban
maisha yake yote lakini kwa sasa amejikita zaidi katika utunzi na utengenezaji
wa nyimbo za Hip Hop, Reggae na ni mzuri katika aina tofauti tofauti za muziki.Pia anapendelea zaidi muziki wa bendi hii ina maana kwamba anataka kuonesha kipaji chake.
Abela hana shida juu
ya kufanya collabo na wasanii wa Kitanzania na Africa kwa ujumla kwa hiyo kama
unapenda kumshirikisha kazi ni kwako! Kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake unaoitwa Ball & Chain.
Kabla ya hapo ametamba
na nyimbo nyingi zikiwemo Rolling Stone, Someone like you na Hey Ya.
Kama unataka kutizama video zake zaidi BOFYA HAPA
Imeandaliwa na Dotto Kahindi
Kama unataka kutizama video zake zaidi BOFYA HAPA
Imeandaliwa na Dotto Kahindi
5 comments:
Tanzania haina dual citizenship...Lakini rahisi kujipatia sifa kutoka kwa ex-citizens.
Low quality music kwa America
SAUTI BADO SANA LOW QUALITY ANAIMBA FLAT SANA
Ni habari njema sana lakini katika mafanikio kama haya anatambulishwa
kwa ukabila na ukwetu ukwetu badala ya kutambulishwa kama mtanzania inatufunza nini sijui? tabia hii ya kumtambulisha mtu kwa ukabila ukabila in direct
This is 'very backward' eti mkoa wa Kagera umefanikiwa? Jamani mmh! Kama alivyoshangaa Nyerere Quote: "Mtanzania wa leo kweli unajitapa kuwa bado unapanda basi la makabila?" Sifa nyingine bwana! badala ya kujisifia utaifa mtu unajisia umimi...
Hivi kuna nchi linajukana kama 'Kagera' kweli? Waswahili husema 'mcheza kwao hutunzwa' kwani mkisema binti ni Mtanzania mtapunguka nini? lakini kama ni raia wa Kagera basi tunawaachia wana Kagera na mafanikio yao:-)
Na wewe Luka wacha michezo yako ya kuminya mawazo ya wengine.
Post a Comment