ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 5, 2015

ABELA KIBIRA MWANAMUZIKI MWENYE ASILI YA TANZANIA ANAYETIKISA AMERIKA KIMUZIKI

Mkoa wa Kagera umebarikiwa kuwa na uwakilishi mzuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya nchi, mfano mzuri ni Mwanamuziki wa kike Abela ambaye ni mzaliwa wa Bukoba Mkoani Kagera anayepeperusha vyema bendera ya Tanzania kimziki huko Amerika anakoishi na kufanya kazi zake za muziki.
Abela Kibira alizaliwa Septemba 22 mwaka 1989 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya Mtanzania Josiah Kibira mzaliwa wa Bukoba Kagera, Tanzania na Mmarekani, Mrs Josiah Kibira.

Mchanganyiko huo wa tamaduni mbili kwa binti huyo ambaye ana kipaji cha utunzi na uimbaji, umemfanya kujimarisha na kujijengea jina katika muziki kutokana na aina ya muziki na manjonjo anayoyafanya katika mzuiki wake kupendwa.

Abela ni mzaliwa wa Bukoba, Tanzania lakini kwa sasa anaishi Minneapolis, Marekani. Binti huyu anasauti nzuri, ya kipekee na ya kuvutia jambo ambalo nyimbo zake nyingi zimekuwa zikipendwa sana

Onyesho lake la kwanza Binti huyu alilifanya kanisani na ndipo kipaji chache kilipojifunua machoni mwa watu wengi na hivyo kuendelea kuimba katika matamasha mbalimbali shuleni na matamasha maalumu.

Abela amekulia katika mji wa Wayzata, Minnesota na alipendwa kutokana na kuwa na uwezo wa ajabu katika kuimba kwaya na matamasha ya pamoja wakati akiwa katika masomo yake ya sekondari na chuo.

Mwaka 2003 baba yake mzazi Mr. Josiah Kibira alimshirikisha katika filamu yake aliyoiita Bongoland, ambapo Abela alitunga wimbo wa kusindikiza filamu hiyo (soundtrack) jambo lililomuongezea uwezo na umaarufu kwa mashabiki Amerika, Afrika na maeneo mengi ulimwenguni.

Abela ambaye bado binti kigoli anayejitambua amekuwa akiiimba na kujifua utumiaji wa sauti takriban maisha yake yote lakini kwa sasa amejikita zaidi katika utunzi na utengenezaji wa nyimbo za Hip Hop, Reggae na ni mzuri katika aina tofauti tofauti za muziki.Pia anapendelea zaidi muziki wa bendi hii ina maana kwamba anataka kuonesha kipaji chake.

Abela hana shida juu ya kufanya collabo na wasanii wa Kitanzania na Africa kwa ujumla kwa hiyo kama unapenda kumshirikisha kazi ni kwako! Kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake unaoitwa Ball & Chain.

Kabla ya hapo ametamba na nyimbo nyingi zikiwemo Rolling Stone, Someone like you na Hey Ya.



Kama unataka kutizama video zake zaidi BOFYA HAPA


Imeandaliwa na Dotto Kahindi

5 comments:

Anonymous said...

Tanzania haina dual citizenship...Lakini rahisi kujipatia sifa kutoka kwa ex-citizens.

Anonymous said...

Low quality music kwa America

Anonymous said...

SAUTI BADO SANA LOW QUALITY ANAIMBA FLAT SANA

Anonymous said...

Ni habari njema sana lakini katika mafanikio kama haya anatambulishwa
kwa ukabila na ukwetu ukwetu badala ya kutambulishwa kama mtanzania inatufunza nini sijui? tabia hii ya kumtambulisha mtu kwa ukabila ukabila in direct

Anonymous said...

This is 'very backward' eti mkoa wa Kagera umefanikiwa? Jamani mmh! Kama alivyoshangaa Nyerere Quote: "Mtanzania wa leo kweli unajitapa kuwa bado unapanda basi la makabila?" Sifa nyingine bwana! badala ya kujisifia utaifa mtu unajisia umimi...

Hivi kuna nchi linajukana kama 'Kagera' kweli? Waswahili husema 'mcheza kwao hutunzwa' kwani mkisema binti ni Mtanzania mtapunguka nini? lakini kama ni raia wa Kagera basi tunawaachia wana Kagera na mafanikio yao:-)

Na wewe Luka wacha michezo yako ya kuminya mawazo ya wengine.