ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 13, 2015

BILA UJANJA HATA UWE NA TABIA NZURI, FIGA BOMBA HUFAI KUWA MKE!

Niwiki nyingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku kama kawaida.Nimshukuru Mungu kwa kila jambo, hasa nimshukuru kwa kunipa kipaji hiki cha kuweza kuwashauri wenzangu juu ya mambo yanayogusa maisha ya kimapenzi.


Si kila mtu anaweza kuifanya kazi hii lakini naamini mimi ni kati ya wachache waliochaguliwa na Mungu kuitelekeza.
Mpenzi msomaji wangu, wiki hii nataka kuzungumzia suala la mwanamke kujitahidi sana kuwa mjanja katika maisha yake na mpenzi au mume wake. Ujanja ninaozungumzia hapa siyo ule ‘ujanjaujanja’ wa kudanganya.

Nazungumzia ujanja wa kujua mbinu sahihi za namna ya kumshika mwenza wako na akakuchukulia wewe ndiyo wewe, wengine hawana lolote. Pia ujanja wa kujitambua, kujua yapi ni sahihi kuyaiga na yapi ya kuachana nayo, akina nani ni marafiki sahihi na nani ni wa kukaa mbali nao.

Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, mapenzi ni sanaa inayohitaji ubunifu na utundu mwingi. Nakasema kwamba, ili uwe mpya kwenye mapenzi lazima ujielimishe kila siku kwa kusoma majarida, magazeti, kuongea na wataalam wa masuala ya mapenzi na kuangalia vipindi vinayohusu mambo ya mapenzi.

Huko utajifunza mengi yatakayokufanya ujue njia sahihi za kupita kuhakikisha unasafiri salama kwenye boti la mahaba na mpenzi wako, na hata kama yatatokea matatizo, yawe ni yale yasiyoepukika.Ukifuatilia sana utagundua kuwa, wanaume siku hizi hawaoi kwa kuangalia tu msichana mwenye tabia nzuri na umbo la kuvutia. Baadhi wanapenda sana kuoa wasichana wajanja, waelewa!

Unajua kwa nini wanaume wanapenda wanawake wajanja? Ni kwa sababu kwa ulimwengu wa kidijitali wanakwepa aibu wanazoweza kuzipata pindi watakapokuwa kwenye uhusiano na washamba.

Washamba mara nyingi huwa ni malimbukeni, hujifunza mambo yasiyokuwa na faida kwa imani kwamba naye ataonekana mtu kati ya watu. Wanawake wa aina hii ni rahisi kuwaingiza wenzi wao katika hasara kubwa. Hawakawii kuiba, ni rahisi kuharibu vitu, wao ni wabadhirifu na wanapenda makuu!

Wanawake malimbukeni huharibika katika vikao vya saluni, kutokana na sifa kubwa ya umbeya kwenye sehemu hizo. Wanaume wasiokuwa na subira hujikuta wakiwapiga teke wenzi wao mapema, mara tu wanapoanza kuhisi nyendo zisizoeleweka kwa wapenzi wao.

Tumekuwa tukishuhudia wanawake malimbukeni wakiiga tabia za ulevi wa pombe au mihadarati kutoka kwa marafiki zao. Wanabadilika na kuwa mafuska kwa kuwapanga mabwana kila kona!

Wanapochombezwa kuwa mwanamke ni lazima awe na buzi la kuchumia pesa ni rahisi kufuata. Matokeo yake hugeuka makahaba wanaolala nyumbani, akitongozwa hakatai ilimradi aahidiwe pesa. Binti mdogo anajihusisha kimapenzi na mtu sawa na babu yake. Mwanamke ukitaka kudumu katika uhusiano lazima uwe mjanja.

GPL

No comments: