ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 13, 2015

PICHA YA MGOMBEA URAIS YAIBULIWA

Mwandishi wetu
NIkama kumekucha! Tayari mbinu za kuchafuana na kupakana matope miongoni mwa wanasiasa waliojitokeza kugombea urais kupitia chama kimoja cha siasa zimeanza kujitokeza baada ya hivi karibuni kuibuliwa kwa picha ya mgombea mmoja wa chama hicho aliyetangaza nia akiwa na hawara ndani ya chumba cha hoteli.

Kuibuliwa kwa picha hiyo kumekuja siku chache kufuatia mgombea huyo kutangaza nia huku akianika kipaumbele chake endapo atapata ridhaa ya wapiga kura kuingia ikulu.

MUDA WA PICHA
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichotinga katika Ofisi za Global Piblishers, Bamaga-Mwenge, inadaiwa kuwa, mheshimiwa huyo (jina tunalo) na mwanamke huyo ambaye si mke wake, walipiga picha hiyo muda mrefu lakini kutokana na duru za kisiasa za uchaguzi mkuu mwaka huu, picha hiyo inaonekana kuwa ‘keki’ kwa wapinzani wake.

“Unajua hii picha ni ya muda mrefu. Mheshimiwa alipiga akiwa na uhusiano na huyu mrembo. Sasa mheshimiwa alipotangaza nia tu, wabaya wake wakaona hapa ndiyo penyewe, wakaiibua ili itumike kwenye kampeni yake ya urais kama chama chake kitampitisha yeye kugombea,” kilisema chanzo hicho.

ENEO LA PICHA

Ilizidi kudaiwa kuwa, picha hiyo ilipigwa ndani ya hoteli moja maarufu iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mpigaji alikuwa mwanamke huyo ambaye hakujulikana jina akitumia simu yake ya mkononi kwa kuishika kwa mkono wake wa kulia (selfie).

SI MKE WAKE
Chanzo kilisema kwa sababu mheshimiwa huyo wa kutoka Kanda ya Ziwa ana mke na watoto na anaheshimika katika jamii, kupiga picha ya namna hiyo kunamuondolea sifa ya kuwa rais wa Tanzania.

“Ingekuwa picha yenyewe ni mheshimiwa na mke wake, sidhani kama wabaya wangeitumia lakini sasa si unajua maadili ya Kiafrika. Nadhani hata wenzetu nje, huwezi kuwa na mke halafu ukawa na hawara wakakupa cheo kikubwa kama cha urais wa nchi,” kilisema chanzo hicho.

HALI ILIVYO KWA SASA
Tayari baadhi ya wagombea wa urais kupitia vyama mbalimbali wameanza kuwalilia baadhi ya wenzao kwamba, wameanza kucheza rafu katika safari ya kinyang’anyiro cha kuusaka urais kwa kuwatafutia skendo chafu, za zamani na mpya ili wachafuke katika jamii na kuonekana hawafai kukabidhiwa ikulu, Oktoba mwaka huu.

ORODHA YA WAGOMBEA
Mpaka sasa, mbali na Chama Cha Cuf ambapo wameshamtaja Profesa Ibrahim Lipumba kugombea urais mwaka huu, wanachama wenye nguvu walioonesha nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Edward Lowassa, Benard Membe, Frederick Sumaye, Samuel Sitta, Makongoro Nyerere, Mwigulu Mchemba, Lazaro Nyalandu, January Makamba.

GPL

No comments: