Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu Dk. Mwale Malecela pichani kabla ya kuingia katika chumba cha habari katika Redio ya Mwambao iliyopo Tanga eneo la Kange ndani ya Kiwanda cha Tanga Fresh ambaye ni mtoto wa Makamu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) John Malecela ni miongoni mwa wana CCM ambao wamejitosa kugombea urais kupitia CCM. Dk. Mwale katika maisha yake mengi kwa zaidi ya miaka20 amekua mtumishu katika Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambako alianza kazi akiwa kijana na akapanda hadi kuwa mtafiti mkuu na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu, licha ya kukulia katika familia ya mwanasiasa.
Dk. Mwale Malecela (kulia) akizungumza na wananchi kupitia kituo cha Mwambao Radio kilichopo Tanga eneo la Kange ndani ya Kiwanda cha Tanga Freshi, kushoto ni mtangazaji wa zam Jonas Msangi
Dk. Mwale Malecela katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Mwambao Radio.(PICHA NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA BLOG.
No comments:
Post a Comment