ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 12, 2015

Dogo Aslay: Nitakupwelepweta Hajaimbiwa Wema Sepetu


Mwanamuziki Aslay Isihaka kutoka katika kundi la Yamoto Band amefunguka na kuweka wazi kuwa anasumbuliwa sana na watoto wa kike ndiyo maana ameamua kuweka mahusiano yake wazi, Aslay alifunguka hayo alipokuwa akichat Live katika kipengele cha Kikaangoni Livekupitia ukurasa wa facebook wa EATV.
Aslay alisema kuwa moja ya sababu iliyomfanya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ni kutaka kutoa ujumbe kwa wale ambao wanamsumbua kuwa waache kufanya hivyo kwani tayari ana mtu ambae yeye anampenda.

"Nimeamua kuweka mahusiano yangu ya mapenzi wazi sababu nasumbuliwa sana, nahisi kufanya hivyo wataelewa na kuacha, yaani kama nimewapunguzia speed ya usumbufu" 
Mbali na hilo Aslay aliweza kuzungumzia juu ya elimu yake na kusema hakuacha shule kwa sababu ya muziki ila ataendelea na shule pale alipoishia, ilaa anaamini atafanya hivyo siku za usoni.


MAHUSIANO YAKE NA WEMA

Tetesi zilizopo mtaani ni kwamba Aslay Isihaka alikuwa akifukuziwa na Wema Sepetu kimapenzi na watu wengi walipouliza swali walitaka kufahamu ukweli juu ya suala hilo na ndipo hapo Aslay alipofunguka na kuweka wazi juu ya suala hilo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote na wimbo wa Nitakupwelepweta hajaimbiwa Wema Sepetu.

"Watu wanakuwa wanaongea mambo mengi juu ya maisha yangu hususani katika mahusiano na kusambaza taarifa zisizo na ukweli, mfano watu wanasema natoka kimapenzi na Wema huo siyo ukweli kabisaa bali Wema ni kama dada yangu, ila kutokana na mambo haya ndipo niliamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kila mtu ajue kuwa nipo kwenye mahusiano na mtu fulani na waache kusambaza taarifa zisizo na ukweli."

Kwa kifupi hizo taarifa wanazosema mashabiki hazina ukweli wowote,kwa sasa nimemtangaza mpenzi wangu na ndiye niko nae, sitaki usumbufu tena kwa sasa.

EATV.TV

1 comment:

Anonymous said...

hizi story ni kweli au ni hekaya za shigongo? wema wema jamani jina lako zuri na una wema kweli lakini mbona unajiharibia sifa yako baby girl kama kuna kaukweli katika story hii.
au ndo katika le projects za kusaka umaarufu na kuza sura na magazeti.mmmh