ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 6, 2015

JENGO SKULI MPYA YA MICHAKAINI WILAYA YA CHAKE CHAKE YAFUNGULIWA RASMI

JENGO la ghorofa moja la skuli mpya ya Michakaini wilaya ya Chake Chake Pemba, ambalo lilijengwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Japan, kabla ya balozi wa nchi hiyo, nchini Tanzania Masaharu Yoshida kulifungua rasmi.
BALOZI wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida akiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla, wakikata utepe kuashiria kulifungua jengo jipya la ghorofa moja la skuli ya Michakaini lililojengwa na serikali ya watu wa Japan.
MWENYEKITI wa kamati ya skuli ya Michakaini wilaya ya Chake Chake Pemba, Nassor Harith akiwa na balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida, wakiitembelea skuli mpya ya ghorofa moja, liliojengwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Japan.
WANAFUNZI wa skuli ya Michakaini wilaya ya Chake Chake Pemba, wakimsikiliza balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida, akizungumza nao mara baada ya kulifungua jengo jipya la ghorofa moja skulini hapo lililojengwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Japan.

 BAADHI ya viongozi wa serikali kisiwani Pemba, waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa skuli mpya ya ghorofa moja yenye vyumba saba vya kusomea, iliojengwa kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Japan, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments: