ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 12, 2015

KADA WA DMV AJIANDIKISHA KUPIGA KURA DODOMA

 Mhudumu wa daftari la kudumu la kupiga kura akiendelea na uandikishwaji wa wapiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu jijini Dodoma nchini Tanzania.
 Mratibu wa matawi ya CCM nchini Marekani Bi.Loveness Mamuya (wapili toka kulia) akiwa kwenye mstari wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.
Mratibu wa matawi ya CCM nchini Marekani Bi.Loveness Mamuya akisubili zamu yake ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura jijini Dodoma mkoa alikozaliwa.

6 comments:

Anonymous said...

hii sasa kali wabunge walisema hawataki uraia pacha, sasa mbona huyo dada anajiandikisha kupiga wakati yeye ana ukazi wa kudumu marekani(maana yake anaelekea kuwa raia wa marekani)!!!! hivi serikali yetu iko makini kweli????

Anonymous said...


Hakuna sehemu kwenya sheria inayomkataza mtu aluyezaliwa Tanzania haki yake ya kupiga kura au uongozi. Shereria zilizopo ni zile zilizandikwa wale wakoloni ambo walikuwa ni wabaguzi na kunyima haki za watu wenye elimu na maendeleo. Huyu Dada Lovelness anafungua mlango kwa watu wote waishio uagibuni-DIASPORA- kuwania haki yao kwa maana unongozi wa nchi unataka viongozi walio kaa nje na kuleta mabadilio nchini kama nchi nyingine duniani. kuendelea zaidi,wapigania Uraisi kuoka Ugaibuni wako kwenye msitari.. Oye Bi. Loveness, Oye CCM,Chadema,CUF, Oye Tanznania

Anonymous said...

Hapo ndo tunapojichanganya mdau. Wapo wenyeviti wengi wa matawi ambao tayari ni raia wa marekani. Ninachoogopa na kuwaonea huruma ni kwamba wanavunja sheria ya marekani na ya Tanzania. Tujielemishe jamani kabla ya kujihusisha na mambo fulani fulani.

Anonymous said...

Wachangiaji mbona mnajichanganya? Huyu siyo rai wa Marekani anajiandikisha kupiga kura halafu kajipiga picha ili apate attention. Halafu hagombei na wala hana uwezo wa uongozi.

Unknown said...

Ki ukweli ni kwamba sisi tunaoishi ughaibuni kama tulizaliwa Tanzania basi tuna haki ya kuitwa hivyo na kama tuna haki ya uraia wa kuzaliwa basi tuna haki ya kupiga kura au kumpigia kura kiongozi tunayemchagua.
Uraia wa American haumzuii mtu kuwa na uraia wa nchi nyingine.

Anonymous said...

nyinyi kweli vilaza, Tanzania haitambui uraia wa nchi nyingine. ukiwa raia wa nchi nyingine au mkazi wa kudumu wa nchi,sheria ya Tanzania iko wazi inabidi uuvue utanzania wako. huyo dada amevunja sharia na serikali ya Tanzania inabidi imchukulie hatua za kisheria kama yule bwana wa kule mbeya alijiandikisha mara mbili. serikali ya jamhuri ya muungano inabidi iwe makini na watu kama hao. katiba yetu ya Tanzania iko wazi kabisa ktk mambo kama haya. ccm huyu mwanachama wenui amevunja sharia sasa tuone mtasema nini kuhusu hili. chadema,cuf,nccr na vyama vingine anzeni kuangalia huu ujanja unaotumika.