Wananchi wa Mji wa Kigoma wakiwa wamejipanga kando ya Barabara kuu ya Kutoka Ujiji, kumpokea Mtangaza nia ya Kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mtangaza nia ya Kuwania Urais kwa tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkoani wana CCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma waliofika kumlaki kwenye Ofisi Kuu za CCM mkoani hapo.
Mh. Lowassa akisani kitabu cha wageni kwenye Ofisi Kuu za CCM Mkoani Kigoma leo, Kulia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC), Daniel Nsanzugwanko.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaborou, muda mfupi kabla ya kupokea idadi ya majina ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amedhaminiwa na wanaCCM 11,250 Mkoani Kigoma, leo Juni 13, 2015.
Wazee kwa vijana wakimshangilia Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinganga, Hamis Mngeja akizungumza machache mbele ya hadhara ya wanaCCM wa Mkoa wa Kigoma.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji akizungumza wakati akimuelezea Mh. Lowassa, idadi ya wanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Noverty Kibaji (kushoto) akimkabidhi, Mh. Edward Lowassa, majina ya wanaCCM wa Kigoma Mjini waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Mh. Lowasaa akionyesha majina ya WanaCCM wa Mkoa wa Kigoma waliomdhani ili aweze kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwania Urais wa Tanzania.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC), Daniel Nsanzugwanko (kulia) amkabidhi Mtangaza nia, Majina ya wanaCCM wengine waliomdhani.
Umati wa WanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Kigoma, ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Kigoma, kuja kumuona Mh. Edward Lowassa (anaeonekana kule mbele) wakati alipofika kuomba udhamini wa wanachama wa CCM, ili aweze kupata ridhaa ya Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhaminiwa na wanaCCM 11,250 wa Mkoa wa Kigoma, leo Juni 13, 2015.
Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM wa Mkoa wa Kigoma.
No comments:
Post a Comment